WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV

WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV
kiungo : WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV

soma pia


WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekutana kujadili suala la ufungaji kamera maalumu za kudhibiti na kuzuia uhalifu. 

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema Serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera hizo katika miji yote mikuu nchini. 

Waziri Masauni alisema lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani, uporaji wa fedha katika taasisi za fedha. 

“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu. 

“Teknokolojia haiepukiki katika kudhibiti, Serikali tumejipanga na hivi karibuni tutaanza kufunga kamera za CCTV katika miji mikuu na maeneo ya mikoa iliyoko mipakani ili kudhibiti wahalifu kutoka nje ya Tanzania,” alisema Masauni 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub alisema tayari washafunga kamera hizo ambazo zilizinduliwa Oktoba 3, mwaka huu. 

Alisema uzinduzi wa kamera hizo ulifanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein. 

“Mfumo huo ni muhimu na tumehakikisha unaimarisha usalama katika mji wa Zanzibar ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na salama na tayari ushaanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa Zanzibar,” alisema.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub (kushoto), wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto).
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto).
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Hivyo makala WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV

yaani makala yote WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wizara-zakutana-kujadili-mfumo-wa_18.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV"

Post a Comment