UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT
kiungo : UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

soma pia


UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Mwinyi ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mitatu ya ujenzi wa Ofisi ya Bunge inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji la Jeshi hilo (SUMA JKT).

Mhe. Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kukagua miradi hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajab Mabele.

“Nimeridhishwa hatua ya utekelezaji wa miradi mitatu inayotekelezwa na SUMA JKT ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi ya Bunge, naishukuru Ofisi ya Bunge kwa kuliamini shirika la SUMA kwa ajili ya kutelekeza miradi hii,” alisema.Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai alilipongeza SUMA JKT kwa kuendelea kutelekeza miradi hiyo kwa ufanisi na kwamba hadi sasa miradi yote inaendelea vizuri.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Bunge, ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa lift na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge.Alisema kwa upande wa ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge tayari SUMA JKT wameshalipwa asilimia 40 na kazi zinaendelea vizuri.

“SUMA JKT ni shirika ambalo tumekuwa tukifanya nalo kazi na tunaridhika na kazi zao tunatamani wapewe miradi mingi ya Serikali,” alisema

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma. Waziri mwinyi ametembelea Ofisi ya Bunge kukagua miradi mitatu 3 ya ujenzi ya inayotekelezwa na Suma JKT. 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia. Nyuma ya Waziri Mwinyi (mwenye miwani ) ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT Kanali Rajab Mabere na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerari Martin Busungu .

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge wakati viongozi hao walipotembelea eneo linapojengwa lift katika Jengo la Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma . 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia.


Hivyo makala UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

yaani makala yote UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/ukaguzi-wa-miradi-ya-bunge.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UKAGUZI WA MIRADI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT"

Post a Comment