title : RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20
kiungo : RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20
RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii
MKURUGENZI wa Fairme NGO, Rene Staheli (62) ambaye pia ni raia wa Uswis leo Oktoba 23.2018 amehukumiwa kulipa faini ya Sh Sh. Milioni 34 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kukiri kosa la kukutwa na vipande vitatu vya meno ya Kiboko.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Rwizile amesema mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kufuatia yeye mwenyewe kukiri kosa lake.
Kufuatia kukiri kutenda kosa linalokukabiki na kukubali vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapa,mahakama inakutia hatiani na inakuhukumu kulipa faini ya Sh 34,036,188 na iwapo utashindwa basi utatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani", amesema Hakimu Rwizile.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita aliiomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshtakiwa huyo kwa kukutwa na maliasili yetu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Katika utetezi wake, ameiomba mahakama impe adhabu ndogo kwa kuwa hili ni kosa lake la kwanza, haijaisumbua mahakama ndio maana amekiri kosa lake na pia anafamilia kubwa inayomtegemea huko kwao Uswisi.
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Oktoba 16, mwaka huu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere alikamatwa akiwa na nyaraka za Serikali ambazo ni vipande vitatu vya meno ya Kiboko vyenye uzito wa kilogeamu tano na thamani ya USD 1,500 ambazo ni sawa na Sh 3, 403, 618.80 Mali ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.
Hivyo makala RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20
yaani makala yote RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/raia-wa-uswisi-ahukumiwa-kulipa-faini.html
0 Response to "RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA KWENDA JELA MIKA 20"
Post a Comment