OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA

OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA
kiungo : OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA

soma pia


OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA


Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki moja kwa mtaalamu Elekezi wa Kampuni ya Archquants Service Limited  kuhakikisha inawasilisha michoro ya kazi za nje ya Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo kilichopo Mkoani Ruvuma ili ujenzi wa chuo hicho uweze kukamilika. 

Mheshimiwa Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa mradi huo. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo. 

Naibu Waziri amesema ukanda wa Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutasaidia wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma na baadae kutekeleza kwa vitendo. 

“Serikali inatilia mkazo Elimu ya ufundi na imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi kupata Elimu ya ufundi na ndio maana Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha 

Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,wakielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.pichani kusho ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa maelezo kuhusina na maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (wa tatu kulia) na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.


Hivyo makala OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA

yaani makala yote OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/ole-nasha-aitaka-veta-kuanzisha-kozi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "OLE NASHA AITAKA VETA KUANZISHA KOZI YA UFUNDI WA ZANA ZA KILIMO SONGEA"

Post a Comment