KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO.

KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO.
kiungo : KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO.

soma pia


KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO.

Baadhi ya Wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Baadhi ya Wazazi wa Wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere wakati wa Mahafali ya watoto wao.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akimkabidhi cheti mwanafunzi bora katika masomo yote wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam, Richard Sagwe wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Bw. Richard Kayombo (kushoto) pamoja na uongozi wa shule ya sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere ameitaka jamii kuendelea na utamaduni wa kutoa na kudai risiti ikiwa ni sehemu ya kuongeza mapato ya Serikali ambapo makusanyo ya kodi hizo hutumika katika kuisaidia jamii katika kufanya maendeleo mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu y shule, barabara pamoja afya.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Mahafali ya shule ya sekondari Misitu iliyopo eneo la Kivule katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo alialikwa kama mgeni rasmi shuleni hapo.

Kamishna Kichere ameeleza kwamba, miongoni mwa changamoto zinazozikabili shule mbalimbali nchini ni vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, madawati, maabara, pamoja vitendea kazi ambapo kupitia ulipaji kodi mzuri ndiyo njia pekee inayoweza kuzitatua kero hizo.

Nimesikiliza risala yenu nikaskia mnashida ya kompyuta, chumba cha kompyuta, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu pamoja na mahitaji mengine, nichukue nafasi hii kuwaeleza kwamba, kuna baadhi ya changamoto ambazo sisi kama Mamlaka hatuna uwezo nazo, lakini tunaweza kuwataftia wafadhili ambao wanaweza kusaidiana na sisi kuzitatua kero hizi, alisema Kichere.

Kichere ameongeza kuwa, anafurahi kuona vijana wengi wanaitikia wito katika kujiunga na vilabu vya kodi katika shule za sekondari ambapo pia ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mashindano ya vilabu vya kodi yaliyofanyika hivi karibuni.

Hawa vijana wetu, baadhi yao walihudhuria katika mashindao ya vilabu vya kodi na walifanya vizuri, mwaka jana niliona wasilisho lao nilifarijika sana kwasababu shule ya sekondari Misitu ilifanya vizuri sana, sisi TRA tumeanzisha vilabu hivi vya kodi kwa lengo la kuwajenga vijana wakiwa wadogo kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ili wao wakawe mabalozi wetu wa kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, alisema Kichere.

Katika hafla hiyo, Kamishna Mkuu ameahidi kuwa Balozi wa shule hiyo na ahadi ya kutoa msaada fedha taslimu shilingi milioni 25 ikiwa ni sehemu ya kuwezesha ujenzi wa chumba maalum cha Kompyuta ambapo kitatumika katika kuwawezesha vijana kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu teknolojia lakini pia waweze kuhamasisha jamii kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Sambamba na wito wa kulipa kodi, Kamishna Kichere ameitaka jamii kulipa kodi mbalimbali pamoja na kuendelea na wito wa kutoa na kudai risiti kwa kila manunuzi wanayofanya.

Akitoa taarifa fupi ya kuanzishwa kwa shule hiyo, Mwalimu Mkuu wa Sekondari Misitu, Bw. Pantaleo Magari alisema kuwa, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi wapatao 1,132 ikiwemo wavulana 577 na wasichana 555 yaani kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.

Aliongeza kuwa, shule kwa sasa ina jumla ya Walimu 39 ambapo kati yao 13 ni wa kiume, 26 wa kike na katika idadi hiyo walimu 29 ni walimu wa masomo ya Sanaa, wawili wa masomo ya biashara na walimu wa masomo ya sayansi wako nane.

“Shule ilipokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wa chagua la pili wapatao 118 ambao hawakupata nafasi katika chagua la kwanza na wakati huo shule hii ilianza chini ya aliyekuwa Kaimu Mkuu wa shule, Bi. Rehema Almas ambaye alipokea wanafunzi hadi kufikia mwezi Septemba, 2017, alisema Magari.

Aliongeza kuwa, mwishoni mwa mwezi Novemba, 2011 yeye ndiyo akawa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo mpaka sasa.

Shule ya sekondari Misitu ilianza mnamo tarehe 16 Aprili, 2017 ikiwa ni miongoni mwa shule zilizojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala maarufu kama shule za kata ambazo zilijengwa kwa kushirikiana na nguvu za wananchi. Shule hiyo kwa sasa ina jumla ya vyumba vya madarasa 16 pamoja na Maabara tatu zikiwemo za kemia, biolojia, na ya fizikia.


Hivyo makala KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO.

yaani makala yote KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/kamishna-mkuu-tra-aipiga-jeki-misitu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAMISHNA MKUU TRA AIPIGA JEKI MISITU SEKONDARI, AAHIDI KUWA BALOZI WAO."

Post a Comment