title : Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu
kiungo : Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu
Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu
Na Lorietha Laurence –WHUSM,Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuitisha kikao na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) pamoja na baadhi ya waandishi wa habari hizo kujadili na kupitia katiba ya chama hicho.
Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo jana Jijini Dar es Salaam alipokutana na baadhi ya Waandishi wa Habari za michezo , alichokiitisha baada ya kupokea barua ya malalamiko zinazoelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi hao wa michezo.
“ Watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa waiteni viongozi wa TASWA wakiwemo na wawakilishi ambao ni waandishi wa habari za michezo ili kupitia katiba inayokiongoza chama hicho kabla ya uchaguzi Mkuu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aliongeza kwa kueleza kuwa waandishi wa habari za michezo wana uhuru wa kuunda chama kipya endapo hawaridhishwi na utendaji wa TASWA ingawa kabla ya kufanya maamuzi yoyote, kikao kifanyike kwanza ili kufikia muafaka.
Alizidi kufafanua kuwa waandishi wa habari za michezo ni muhimili muhimu katika sekta ya habari na maendeleao ya michezo ndani na nje ya nchi, kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha jamii kuhusiana na masuala ya michezo.
Wakati huo huo, Dkt. Mwakyembe alipata nafasi ya kutembelea wasanii wa kikundi cha Nafasi Arts Space kilichopo Mikocheni B Jijini Dar es Salaam, ambapo alifurahishwa na kazi mbalimbali za sanaa zinazofanywa na kikundi hicho.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari za michezo kilichofanyika jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari za michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika picha) katika kikao kilichofanyika jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akipata maelekezo kutoka kwa Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Bw. Ramadhani Mabera (kushoto) na kulia ni Mwalimu wa Sanaa za Uchoraji kutoka Zanzibar Bw. Abdulla Omar maarufu kama Dulla Wise.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akipokea zawadi ya picha ya kuchora kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Nafasi Arts Space Bibi. Sauda Simba baaada ya kuzungumza na wasanii hao jana Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu
yaani makala yote Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dkt-mwakyembe-bmt-waiteni-taswa.html
0 Response to "Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu"
Post a Comment