title : Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama.
kiungo : Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama.
Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akifungua Semina ya Siku moja ya Mafunzo ya kuwejengea uwezo Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusiana Sheria ya Usimamizi wa Mahkama, mkutano huo umefanyika katika ukumbi w Wizara hiyo mazizini Zanzibar.
Na.Raya Hamad OR KSUUUB
Mapendekezo ya Sheria ya usimamizi wa Mahakama yataongeza kasi ya uwajibikaji kwa watendaji wa Mahakama na kupelekea upatikanaji wa huduma bora kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar.
Waziri wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh Haroun Ali Suleiman ameleza hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwelewa kuhusu mswada wa sheria , uliwashirikisha Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Baraza la Wawakilishi na Makatibu wao .
Mheshimiwa Haroun amesema Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeamuwa kupendekeza sheria hii kwa msingi wa utekelezaji wa program ya mageuzi katika sekta ya sheria kama ilivyobainiwa kwenye mkakati wa tatu wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Zanzibar pamoja na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020 kuhusu kuimarisha utawala bora wa sheria .
Aidha amesisitiza kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuimarisha Utawala bora na kuhakikisha kuwa Mahakama inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na nidhamu , uadilifu usawa na uwazi ili kutimiza mahitaji ya wananchi na kusisitiza kuwa mapendekezo ya sheria ya usimamizi wa Mahakama yataongeza kasi ya uwajibikaji kwa watendaji wa Mahakama na kupelekea upatikanaji wa huduma bora kwa wakati na kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar
Nae Naibu Katibu anaechughulikia Katiba Sheria Nd George Kazi amesema bado kuna changamoto kwa maendeleo ya mahakama kwa baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo haijapata kutekelezeka ili ufanisi wa kazi na maendeleo ya Mahakama uweze kupatikana ni vyema kuzitofautisha kazi za Mrajis na kuwa na Mtendaji wa Mahakama
“ katika utafiti uliofanyika imeonekana kunahitajika kuwa na utaratibu tofauti na uliopo wasasa ili kuwepo na maendeleo hivyo kutofautisha kazi za utawala utumishi,masuala maendeleo na sehemu itakayoangalia masuala ya mahakama na utowaji wa haki hivyo tuliona ni vyema kuangalia kwa wenzetu mabadiliko gani waliyoyafanya na kuweza kufikia malengo zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia na nyenginezo
Maadili ya watu wa Mahakama ni tofauti na maadili ya taasisi nyengine kulingana na mazingira hivyo basi sheria hii inayopendekezwa imekuja kwa ajili ya kulinda maadili, heshima na uelewa wa kazi za majaji pamoja na watendaji wengine .
Tunategemea kuwa na mfuko wa Mahakama, uwepo wa mfuko huo utawezesha pia washirika wa maendeleo kuweza kuingiza fedha moja kwa moja kwa mfuko ili Mahakama iwe inaweza kujitegemea
Akitowa mada muwezeshaji wa semina hio Mwanasheria wa Serikali Nd Saleh Said Mubarak amefafanuwa kuwa Jaji Mkuu atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi za Mahakama zikiwemo utoaji wa maelekezo, usimamizi wa vikao vya Mahakama na ugawaji wa majukumu ya Mahakama
Aidha Jaji Mkuu atakuwa Mkuu wa Mahakama na pamoja na kazi zilizoelezwa katika Katiba au sheria nyengine yoyote, atatekeleza kazi na mamlaka yaliyoelezwa katika sheria pendekezwa
Kwa upande wa Mrajis atawajibika kwa Jaji Mkuu kwa utekelezaji bora wa kazi za Mahakama na kufafanua kazi za Mrajis ni kuwezesha na kusimamia utekelezaji wa kazi za Mahakama , kuratibu shughuli za Mahakama kutoa taarifa ya jumla ya utekelezaji wa kazi za Mahakama, kuwa kiunganishi baina ya Mahakama na Tume katika uteuzi, upandishaji vyeo na mambo ya kinidhamu ya Majaji, Mahakimu na Makadhi, atawasiliana na Serikali kuhusiana na mambo yanayohusu taaluma ya Mahakama au mambo mengine yoyote ambayo Serikali inaweza kuhusika .
Semina hio ilifungwa na Naibu Waziri wa wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Khamis Juma Mwalim ambapo amesisitiza uelewa wa mswada wa sheria hii utasaidia katika suala la kuendeleza utawala bora katika Taasisi za Sheria
Mswada wa Sheria ya kuweka masharti bora ya usimamizi wa Mahakama kufafanua Utumishi wa Mahakama kuanzisha Ofisi za Mtendaji Mkuu wa Mahakama na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo utajulikana kama Sheria yaUsimamizi wa Mahakama 2018 utawasilishwa na kusomwa mara ya pili na kujadiliwa Baraza la Wawakilishi na kisha kuanza kutumika mara baada ya kutiwa saini na Rais .
Hivyo makala Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama.
yaani makala yote Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wenyeviti-wa-kamati-za-baraza-la.html
0 Response to "Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama."
Post a Comment