Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola

Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola
kiungo : Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola

soma pia


Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola



WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kuchukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, imeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu katika hotuba yake kwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini yaliyoanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo imesharipotiwa ugonjwa huo umeingia nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Mhe. Mwalimu amesema TAA inafanya jambo jema kwa kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege wanafanyiwa ukaguzi na kutoa taarifa za afya zao kwa wale ambao watabainika kuwa na joto la mwili lisilokuwa la kawaida.

“Nawapongeza sana tena sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama bila kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa Ebola, imeripotiwa sasa huu ugonjwa upo Kivu Kaskazini, ambapo ni karibu na nchini na Wavuvi wanakuwa na muingiliano kwa kutoka huko na kuja nchini,” amesema Mhe. Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akiongea na wananchi walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
DSC_0783Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akikata utepe kuzindua kitabu cha mpango mkakati wa udhibiti wa ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, baada ya kufanya Matembezi ya Hiyari yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa Ebola.
DSC_2006Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela akiongea na wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa kuanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Viwanja vya Karimjee.
DSC_0608Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (watatu kulia) leo akiongoza Matembezi ya Hiyari kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mohamed Kambi.
DSC_1935Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa miongoni mwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola

yaani makala yote Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-ummy-avipongeza-viwanja-vya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola"

Post a Comment