title : Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini
kiungo : Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini
Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini
WAANDISHI wa Habari wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuihabarisha jamii ili kuepukana na janga hatari la ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameyabainisha hayo wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa waandishi wa namna ya kutoa taarifa za ugonjwa huo wa Ebola.
Jamii imetakiwa kujua dalili za ugonjwa huo wa Ebola kwa kina kwani kupitia Wanahabari,mafunzo hayo yatasaidia sana kutoa elimu na itaenea maeneo mengi.
“Ugonjwa huu wa Ebola kiukweli ni ugonjwa hatari. Na tokea kutokea katika nchi za wenzetu umesababisha madhara makubwa sana ikiwemo Uchumi ikiwemo masuala ya biashara na uwekezaji.
Imebainishwa kuwa madhara ya kiuchumi juu ya Ebola yangeuwa watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wenyewe. Sisi tulikuwa na wasiwasi sana ndio maana tulienda wenyewe huko kufuatilia..mimi nilienda mipakani Rusumo na Mganga Mkuu yeye alienda mipaka ya Ngala na maeneo mengine.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Na kuongeza kuwa, tatizo kubwa ni suala la wasafiri wanaopita njia za panya kwani zimekuwa zikiwapa changamoto na wameomba Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda maeneo hayo.
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa Semina jinsi ya kurepot Kuhusu ugonjwa wa Ebola na namna ya kuzuia usiingie nchini.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze Akizungumza na waandishi wa habari kuhusukushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa huo wa Ebola ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika leo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini
yaani makala yote Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wanahabari-wafundwa-juu-ya-mlipuko-wa.html
0 Response to "Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini"
Post a Comment