title : WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU
kiungo : WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU
WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU
Wakala wa Manispaa ya Jiji la Arusha Robert Modu akiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu leo kabla ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kugushi na kutoa nyaraka za uongo na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 23 kwa njia ya udanganyifu.
Wakala wa Manispaa ya Jiji la Arusha Robert Modu akitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kugushi na kutoa nyaraka za uongo na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 23 kwa njia ya udanganyifu.
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
WAKALA wa Manispaa ya Jiji la Arusha Robert Modu, leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kugushi, kutoa nyaraka za uongo na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 23 kwa njia ya udanganyifu.
Akisoma hati ya mashtaka leo mahakamani hapo Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leornad Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Wanjah Hamza kuwa, mshtakiwa ametenda makosa hayo kati ya Desemba 4 mwaka 2013 na Julai 14 mwaka 2014 huko Kijitonyama.
Imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa Modu kwa nia ovu alitengeneza nyaraka ya uongo ya hati ya madai yenye kumbu kumbu RA/CC &ADV/VOL.1/1078 kwa madai kuwa hati hiyo ilitolewa na Manispaa ya Jiji la Arusha huku akijua kuwa si kweli.
Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, tarehe hizo katika ofisi za Kampuni ya Sigara Tanzania iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa aliwasilisha hati hiyo ya madai ya uongo yenye kumbu kumbu namba hiyo hiyo, katika kampuni ya Sigara kuonesha kuwa hati hiyo imetolewa na Manispaa ya jiji la Arusha.
Aidha imedaiwa, kati ya Novemba 4 mwaka 2013 na Julai 14 mwaka 2014, katika kampuni ya Sigara ya Dar es Salaam akiwa Wakala wa Manispaa ya Mji wa Arusha kwa nia ya kudanganya alijipatia Sh. 23,273,632 kwa niaba ya manispaa hiyo ya Arusha.
Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alijipatia malipo hayo kuonesha kuwa yameizinishwa na Manispaa hiyo na kwamba fedha hizo alizipokea Kwa niaba ya Manispaa.
Hata hivyo. Mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo na huko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Hamza alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini Wawili wataosaini bondi ya sh. milioni 10 na mmoja kati ya wadhamini hao wametakiwa kiwasilisha fedha Sh. milioni 10 au hati ya mali isiyohamishika yenye kiasi hicho cha fedha.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19 mwaka 2018.
Hivyo makala WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU
yaani makala yote WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wakala-wa-manispaa-jiji-la-arusha.html
0 Response to "WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU"
Post a Comment