Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani

Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani
kiungo : Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani

soma pia


Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani

Na Karama Kenyunko,blogu ya Jamii.

ASKARI Mgambo wawili na Afisa mtendaji wa kata ya Bunju, 
 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumjeruhi kwa kutumia Rungu mkazi wa Bunju Robinson Olotho.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni askari Mgambo Kelvin Sawala (25) na Goodluck Tarimo (30) ambao wanashtakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Ibrahim Mabewa (39).

Wakisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde imedaiwa August 30, 2018 huko  Bunju Wilayani Kinondoni, washtakiwa hao walimpiga Olotho kwa kutumia rungu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali

Hata hivyo washtakiwa wamekana kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya wakili wa serikali, Nassoro Katuga kuieleza mahakama kuwa, licha ya kesi hiyo kudhaminika lakini wanaiomba mahakama isubirishe dhamana ya washtakiwa hao kwa sababu kuu mbili.

Amezitaja sababu hizo  kuwa kuna suala la kiusalama ambapo washtakiwa walionekana kwenye video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, hivyo kama watapatiwa dhamana usalama wao utakuwa shakani kwa sababu wananchi na ndugu wa mjeruhiwa watakuwa na hasira.
Pia akadai sababu nyingine ni kwamba mjeruhiwa bado yupo hospitali na hali yake ya kiafya sio nzuri.

Hakimu Kasonde alipowauliza washtakiwa hao kuhusu hoja hizo walidai hali ya afya ya mjeruhiwa walionana naye jana na anaendelea vizuri wala hayupo hospitalini na kuwa suala la usalama wao liko vizuri, hivyo wanaomba dhamana, 

Hata hivyo, Hakimu Kasonde amesema mahakama imekubali hoja za upande wa mashtaka kuhusu usalama wa washtakiwa hao, hivyo wananyimwa dhamana hadi hapo itakapojiridhisha kuhusu usalama wao.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado hayjakamilika na imeahirishwa hadi September 20,2018.


Hivyo makala Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani

yaani makala yote Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mgambo-wanaodaiwa-kupiga-raia-virungu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani"

Post a Comment