title : HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA
kiungo : HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA
HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA
Khadija Seif, Globu ya jamii
STAA mwenye ubora wake katika tasnia ya filamu za kibongo a.k.a Bongo Muvie Chiki Mchoma amewashauri wasanii wanaochipukia kuhakikisha wanaishi maisha yao halisi.
Amesema hata yeye pamoja waigizaji wengine wengi wakongwe wameishi maisha ya kawaida na kujenga heshima kwa wadau.
Chiki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anapiga stori na Micbuzi Blog ambayo imekutana na Staa huyo na kuzungumza mambo kadhaa kuhusu sanaa ya uigizaji nchini.
Amesema changamoto inayowakumba kwa sasa wasanii chipukizi ni kutopitia makundi mbalimbali ya filamu kama vile zamani wasanii ambavyo wamepitia na kujifunza vingi kuhusu uigizaji.
Amefafanua kupitia makundi hayo waigizaji wengi wamepata elimu, uzoefu pamoja na tabia njema na matokeo yake wamejijengea heshima katika jamii na tasnia ya filamu kwa ujumla.
Pia Mchoma amesema kuna baadhi ya wasanii kwa sasa wanaishi kwa kutegemea kiki wakiamini ndio zinaweza kuwapatia umaarufu badala ya kuweka jitihada kwa kutengeneza kazi nzuri.
Ameongeza uzoefu wao ndio umeweza kuwajenga hivyo basi wajitahidi kujenga heshima ili waheshimike kwa watazamaji pamoja na wadau wa filamu.
"Kwa mataifa ya nje msanii akifanya jambo ambalo halipendezi kwa jamii anachukuliwa hatua kali tofauti na hapa kwetu linachukuliwa ni jambo la kawaida," amesema.
Amewataka wanahabari waelekeze nguvu nyingi kwenye kutangaza kazi zao kuliko kuwatengenezea chuki baina ya msanii kwa msanii au kikundi fulani cha watu.
Ametoa mwito kwa wasanii wanaotegemea Kiki kuwa hazitawajengea chochote badala yake zitafanya wanajamii kuiga mambo ambayo yatawapotosha kwani wasanii ni kioo cha jamii .
Na kwamba chochote watakachokifanya wapo watu ambao wanawatazamaa au kuyafata.
Hivyo makala HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA
yaani makala yote HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/huu-ndio-ujumbe-wa-chiki-kwa-wasanii.html
0 Response to "HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA"
Post a Comment