title : Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito.
kiungo : Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito.
Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito.
Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar. 6-8-2018.
Elimu zaidi inahitajika kwenye Kitengo cha huduma ya
mama na mtoto ili kupunguza vifo mama wajawazito wakati
wa kujifungua na watoto wachanga ambapo takwimu
zinaonyesha vifo 1,091 vya watoto wachanga na 49 vya uzazi
vilitokea katika kipindi cha mwezi Julai 2017 hadi Juni 2018 .
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa
kipindi cha 2017/2018 kwa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya
Baraza la Wawakilishi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Asha
Ali Abdulla alisema sababu kuu ya vifo vya uzazi vinatokana
na uelewa mdogo wa kinmama juu ya umuhimu wa
kujifungulia hospitali na kuchelewa kufanya maamuzi ya
kujifungulia hospitali.
Katibu Mkuu alizitaja sababu nyengine za kitaalamu
zilizopelekea kutokea vifo hivyo ni kifafa cha mimba
kinachosababishwa na sindikzo la damu, kupasuka kwa fuko
la uzazi kunakopelekea kupoteza damu nyingi na
maambukizi kabla na baada ya kujifungua.
Alisema Wizara ya Afya inaendelea kusimamia na kuratibu
shughuli za huduma za mama wajawazito na watoto ili
kuona wanapata huduma bora ambapo katika kipindi cha
mwaka 2017/2018 jumla ya wajawazito
94.181 waliohudhuria klinik angalau mara moja kabla ya
kujifungua.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya alisema katika juhudi za Wizara
hiyo kuimarisha huduma za afya ya uzazi na watoto
wachanga, vifo vyote vinavyotokea hufanyiwa uhakiki ili
kujua sababu yake na kutafuta mbinu za kupunguza vifo
vinavyoweza kuepukika.
Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la
Wawakilishi baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea vituo
mbali mbali vya afya walieleza kuridhishwa na huduma bora
zinazotolewa na watendaji pamoja na kuimarishwa vituo
vingi vya afya.
“Tumeshuhudia huduma zinatolewa kwa kiwango kizuri na
zinaridhisha, watendaji wanafanya majukumu yao kama
inavyotakiwa, dawa na vifaa vinaridhisha kwenye vituo vingi
tulivyotembelea”, alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi
wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Mwanasha Khamis Juma.
Hata hivyo walisema Changamoto kubwa walioiona ni
upungufu wa Madaktari Hospitali Kuu ya Mnazimmoja,
uhaba wa wafanyakazi kwa baadhi ya vituo vya afya na
sehemu za uhifadhi wa dawa haziridhishi na kunaweza
kusababishia uharibifu wa dawa zinapatikana kwa gharama
kubwa.
Wajumbe wa Kamati hiyo wameishauri Wizara ya Afya
kufanya juhudi za makusudi kuongeza Madaktari, Wauguzi
na Wakunga katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na vituo
vya afya vya vijijini ili kazi za kuwahudumia wananchi ziwe
na ufanisi mkubwa zaidi.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Hivyo makala Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito.
yaani makala yote Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/elimu-ya-zaidi-inahitajika-katika.html
0 Response to "Elimu ya Zaidi Inahitajika Katika Huduma ya Mama na Mtoto Kupunguza Vifo Mama Wajawazito."
Post a Comment