DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU.

DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU.
kiungo : DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU.

soma pia


DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva akipokea zawadi kutoka kwa wadau walioshirikia katika uzinduzi wa kampeni katika mkoa wa Dar es Salaam ya Furaha Yangu.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupima ugonjwa wa ukimwi jambo ambalo litasaidia kuzuia maambukizi mapya pamoja na kuishi kwa Furaha.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kupima ugonjwa wa ukimwi inayojulikana kwa jina la 'Afya Yangu' katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva, amesema wakati wote wanatakiwa kupima ugonjwa wa Ukimwi.

Lyaviva ambaye alikuwa anamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amesema kuwa mtu akipima afya yake itamsaidia kujitambua na kuishi kwa furaha pamoja na kuanzishiwa sawa ya VVU na na kusaidia kuzuia maambukizi mapya.

"Naomba wanaume wote wakapime ukimwi kwani takwimu zinaonesha wanaume wengi hawapendi kupima" amesema Lyaviva.

Amesema kuwa baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya upimaji wa ukimwi leo, sasa kila wilaya inatakiwa kuzindua kampeni yake ili kuhakikisha kila mtu anapina na kujua afya yake.

"Kila wilaya inatakiwa kuzindua kampeni yake, kama ikiwezekana baada ya wilaya na ngazi ya kata na mtaa, kufanya hivyo itasaidia kila mmoja kujua afya yake na kupungusha idadi ya maambukizi" amesema Lyaviva.

Lyaviva amefafanua kuwa serikali inaendelea na jitihada kupanga mikakati ya kuzuia maambukizi mapya ya VVU pamoja kuhakikisha kila hospitali zinapatikana dawa za ARV.

"Mbinu za kutopata ugonjwa wa Ukimwi ni kuacha zinaa pamoja na kuwa mcha mungu kama vitabu vya dini vinavyoeeleza" amesema Lyaviva.
Mkazi wa Dar es Salaam akipata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa afya baada ya kupima VVU.
Picha ya pamoja viongozi wa tasisis mbalimbali wakiwa na mgeni rasim Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe, ameeleza kuwa kwa mujibu takwimu za mwaka 20I6 hadi 20I7 maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi umepungua kutoka asilimia 7 hadi kufika asilimia 4.7.

Dkt. Magembe amesema kuwa licha ya kupunguza kwa maambukizi ya VVU katika mkoa wa Dar es Salaam baadhi ya maeneo yameonekana bado yapo juu katika maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Dkt. Magembe ameyataja baadhi ya maeneo hayo ni Mbagala, Kimara pamoja na Buguruni ambayo yameonekana bado hatupo salama.

"Bila kuchukua hatua za haraka kuna Habari ya maambukizi yakaongezeka katika mkoa wa Dar es Salaam" amesema Dkt. Magembe.

Katika hatua nyengine Dkt. Magembe amesema kuwa bado mkoa wa Dar es unaendelea na jitihada za kuhakikisha wanapungunza maambukizi ya VVU.

Amesema kuwa ili kufikia malengo kwa sasa kila mama majamzito amekuwa akipimwa VVU ili kumkinga mtoto wake asipate maambukizi pamoja na kuanzisha utaratibu wa kupewa dawa kwa wale unaogundulika wana maambukizi baada ya kupima afya zao.

Kampeni ya afya yako Mkoa wa Dar es Salaam umezinduliwa leo katika Viwanjwa vya Mbagala Zakhemu huku idadi ya watu zaidi ya I,000 walijitokeza kupima afya zao.

kuanzia septemba 5 hadi 6 mwaka huu katika viwanjwa vya Zakhemu asilimia 60 ya wanaume wamejitokeza kupima VVU huku Wanawake wakiwa asilimia 40.


Hivyo makala DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU.

yaani makala yote DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dar-yazindua-kampeni-ya-upimaji-wa-vvu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DAR YAZINDUA KAMPENI YA UPIMAJI WA VVU YA FURAHA YANGU."

Post a Comment