CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA.

CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA.
kiungo : CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA.

soma pia


CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA.


Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)/Jimbo la Ukonga Mwita Waitara akicheza ngoma baada ya kuwasili katika kampeni katika hilo leo jijini Dar wa Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM)  Dkt. Bashiru Ally pamoja na wabunge wa leo wamefunga kampeni za uchaguzi mdogo akiwa  katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, huku wakitaka wananchi kumchagua mgombea wa Ubunge katika Jimbo hilo Mwita Waitara katika uchaguzi utakaofanyika Septemba I6 mwaka huu.

Akizungumza katika Mkutano wa kufunga Kampeni za CCM leo jijini Dar es Salaam Dkt. Bashiru, amesema kuwa wananchi wa Jimbo la Ukonga wanapaswa kuendelea kumuamini kwa kumchagua Waitara katika uchaguzi utakofanyika kesho.

Amesema kuwa Waitara ni kiongozi mchapa kazi kwani ameanza kumjua tangu akiwa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

"Waitara ni kiongozi mzuri akiwa chuo alifanya vizuri kwa kuwaongaza wanafunzi wezake na bila kupinduliwa muda wote katika uongozi wake akiwa Chuo" amesema Dkt. Bashiru.

Ameeleza kuwa ni mtu makini katika utendaji wake na bila shaka atendelea kulitumikia taifa la Tanzania katika Jimbo la ukonga.

Amesema kuwa CCM itaendelea kutekeleza Ilani yake kwa vitendo ili kuhakikisha inaleta maendeleo na kuamnini.

"Kuna miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM ambayo itasaidia kuinua  uchumi wa Tanzania" amesema Dk. Bashiru.

Katika hatua nyengine Dkt. Bashiru amesema kuwa ndani ya CCM kulikuwa na baadhi ya watu wanatumia fedha zao kupata cheo, lakini kwa sasa uwezo wa mtu ndio anapewa kipaombele katika nafasi mbalimbali za uongozi wake.

"Tunataka kujenga Chama ambacho kinajitegema kifedha na sio kutegemea  wafadhili ambao wamekuwa wakila  rushwa"amesema Dkt. Bashiru.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, amesema kuwa katika uchaguzi utakofanyika kesho amejipanga kuimarisha ulinzi kila mahali ili kuhakikisha wapiga kula wanamchagua kiongozi wanampenda katika hali amani.

Mhe. Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa ulinzi Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kupiga kula bila kuwa na hofu yoyote katika  uchaguzi Chuo.

"Tumejipanga kuweka ulinzi hivyo msiwe na shaka wala hofu, naomba mjitokeze katika vituo vya kupiga kula" amesema Mhe. Makonda.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, amesema kuwa wilaya yake imejipanga kila idara ili kuhakikisha amani inatawala katika uchaguzi huo utakaofanyika kesho.

Mhe. Mjema amesema watu wanapaswa kuondoa hofu na kujitokeza kumchagua kiongozi.

"Tumejipanga kuhakikisha ulinzi unakuwa katika maeneo yote, wapigakula baada ya kupiga rudini nyumani kazi ya kulinda kula wachieni mawakala" amesema Sophia Mjema.

Kwa upande wake Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, amewata wananchi wa jimbo hilo kumchangua tena ili kuendelea kuwalete maendeleo.

Waitara amesema kuwa ameamua kiludi CCM kutokana na utendaji wa Rais Dkt. Magufuli kwani anaamini maendeleo akiwa ndani ya CCM kila kitu kitakwenda sawa katika Jimbo la ukonga.


Hivyo makala CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA.

yaani makala yote CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/ccm-yapigilia-msumari-wa-mwisho-kampeni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CCM YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KAMPENI JIMBO LA UKONGA."

Post a Comment