title : BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA
kiungo : BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA
BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA
Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti akibadilishana nyaraka na kupngezwa na aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo Bwana Patrick Mvungi (kulia) baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitatu. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Katibu mpya wa Baraza hilo Bi. Everlyne Machumu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (Kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimpongeza na kumkaribisha Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti baada ya kuchaguliwa kwenye Baraza hilo la Nne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba ya ufunguzi wa Baraza hilo la Nne la Wafanyakazi wa MOI, Kushoto kwake ni Katibu mpya wa Baraza hilo Bwana Ngina Mitti na kulia ni Naibu Katibu wa Baraza Bi. Everlyne Maachumu.
Picha ya pamoja ya Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya MOI wakati wa Baraza la nne lililofunguliwa rasmi leo Septemba 22 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface katika ukumbi wa mikutano wa IDDI NYUNDO, Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (Kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimpongeza na kumkaribisha Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti baada ya kuchaguliwa kwenye Baraza hilo la Nne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba ya ufunguzi wa Baraza hilo la Nne la Wafanyakazi wa MOI, Kushoto kwake ni Katibu mpya wa Baraza hilo Bwana Ngina Mitti na kulia ni Naibu Katibu wa Baraza Bi. Everlyne Maachumu.
Na.Andrew Chale -Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na
upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk
Respicious Lwezimula Boniface amefungua rasmi Baraza la
Nne la Wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa IDDI
NYUNDO, Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Dkt. Respicious Boniface amefungua baraza hilo kwa
kumwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI, Bi.
Zakia Meghji ambapo vikao hivyo vitafanyika kwa muda wa
siku tatu huku Wajumbe kutoka katika kila idara, vitengo na
chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE),Wajumbe wa
TUGHE mkoa huku kwa upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu-
Utumishi ikiwakilishwa na Bi.Tulia Msemwa.
Akizindua Baraza hilo Dkt. Boniface kwanza alitoa pole kwa
tukio la ajali ya kuzama kwa kivuko kilichotokea kwenye
Ziwa Tanganyika cha MV Nyerere na kupoteza watu wengi
huku pia ametoa pole kwa Rais na Watanzania wote.
Aidha akizungumza kwenye ufunguzi huo, Dk. Boniface
amesema kuwa Taasisi hiyo imenufaika na mageuzi
makubwa katika kipindi cha miaka mitatu kwa huduma
zimeboreka sana na zaidi ya Wagonjwa wa nje (Outpatient)
zaidi ya Laki mbili wamehudumiwa katika kipindi cha
mwaka wa fedha 2017/18.
“MOI ni ‘high Class Hospital, na huduma zetu ni bora sana
ukilinganisha na Hospitali nyingine hapa Nchini na Nchi za
Afrika Mashariki na Kati” Alisema Dkt. Boniface.
Dkt. Boniface amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha
Watanzania wote wanapata huduma zote hapa ambapo kwa
hilo Nchi imefanikiwa sana.
“Kwa upande wa mifupa na ajali tuko vizuri na hakuna
anayekwenda nje ya Nchi. Ila kwa upande wa upasuaji wa
Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kuna wachache
wanakwenda ila Serikali inaliangalia hilo na vifaa
vimenunuliwa na hakuna atakayekwenda nje ya Nchi tena.
Fedha za kununulia vifaa zilitolewa na Serikali yetu sikivu
kiasi cha Tsh. 16.5 Bilioni ambazo zimeiwezesha MOI kuwa
na vifaa vya kisasa vya MRI, CT-SCAN, X-ray, Utra Sound,
na vingine vya kazi muhimu kwa matatizo hayo hivyo Baraza
hili liwe chachu ya kukuwa kwa taasisi yetu.” Alisema Dkt.
Boniface.
Aidha, Dkt. Boniface ameongeza kuwa, kwa sasa wanataka
kupunguza msongamano wa kwa wagonjwa wa
nje wanaofika kupatiwa matibabu ya kliniki kwa kujenga
jengo la kisasa huku pia mpango huo ni pamoja na
kuanzisha mfumo maalum wa wagonjwa kufanya mihadi ya
kuonana na Daktari kwa njia ya mtandao.
“Tunataka tuanzishe ‘propper data base’ ya uhakika yaani
kila anayeingia anajulikana na anaonekana ili kuondoa ili
suala la wagonjwa kuwahi namba hapa ambapo wanakuja
kuanzia saa 12 alfajili hii sasa itakoma. Mfumo huu
utasaidia sana hivyo kwa sasa tunajipanga kwa hilo na
watalaam nimeshaongea nao” alimalizia Dkt. Boniface.
Katika hatua nyingine, Baraza hilo liliweza kupata Katibu
mpya Bwana Ngina Mitti huku Msaidizi wake Bi. Evelyne
Machumu baada ya aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo Bwana
Patrick Mvungi kumaliza muda wake.
Baraza hilo la Wafanyakazi limehudhuliwa na wajumbe zaidi
ya 70 huku pia pia wadau mbalimbali wakiwemo SSRA
ambao walitoa mada juu ya kuunganishwa kwa mifuko ya
hifadhi ya Jamii sambamba na Benki ya NMB ambao ni
waadu wakubwa wa MOI ambao walitoa elimu na mafunzo
namna ya benki hiyo inavyoweza kuwasaidia wateja wake
wakiwemo wafanyakazi wa MOI.
Hivyo makala BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA
yaani makala yote BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/baraza-la-nne-la-wafanyakazi-moi.html
0 Response to "BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA"
Post a Comment