ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO.

ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO.
kiungo : ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO.

soma pia


ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO.


Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, unatarajiwa kuzikwa leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake ulikuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu.

Viongozi kadhaa wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.

Kofi Annan alishika nafasi hiyo akiwa Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.

Leo ni kilele cha wiki kadhaa za maandalizi ya maziko yake akiwa mmoja wa wanadiplomasia walioheshimika duniani.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Accra amesema ngoma za maombolezo zilisikika mfululizo kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Accra, sehemu ambayo mwili wake ulikuwa ukiagwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa waombolezaji waliwasili mjini humo ni aliyewahi kuwa mke wa rais wa kwanza wa Afrika kusini Nelson Mandela, Bibi Graca Machel.

Marais na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo Ivory Coast, Ethiopia na Zimbabwe watahudhuria maziko hayo.

Pia wamo marais wa zamani wa Ujerumani, Finland na Uswizi.


Shughuli hiyo ya kumuaga marehemu itafuatiwa na maziko yatakayofanywa kwa ndugu wa karibu na kwa heshima zote za kijeshi.


Hivyo makala ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO.

yaani makala yote ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/aliyekuwa-katibu-mkuu-un-kuzikwa-leo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ALIYEKUWA KATIBU MKUU UN KUZIKWA LEO."

Post a Comment