ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI

ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI
kiungo : ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI

soma pia


ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI

SEKTA ya kilimo ni mhimili wa uchumi wa Taifa na inategemewa katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025, kupitia viwanda kwa sababu kilimo ndicho kitawezesha viwanda kwa kuvipatia malighafi.

Kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa nchini, serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhakikisha inaiboresha ili iweze kuwa na tija na kufikia malengo iliyojiwekea.

Sekta hiyo mbali na kuwa mhimili wa uchumi wa Taifa, pia imekuwa ikichangia pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za kigeni.

Kufuatia hali hiyo, Serikali imeweka msisitizo katika kusimamia mazao makuu matato ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku ambayo uzalishaji wake umeonyesha tija.

Baada ya kupata mafanikio katika mazao hayo Serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha mazao ya alizeti, ufuta, michikichi ili kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa kutumia mazao hayo na mbegu za pamba.

Itakumbukwa kwamba kila mwaka, Serikali inatumia sh. bilioni 600 kwa ajili ya kuagiza mafuta ghafi ya kula kutoka nje ili kukidhi mahitaji kwa kuwa kiwango kinachozalishwa nchini hakitoshi.

Katika kuhakikisha kuwa jambo hilo linafanikiwa Serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli imeamua kuanzisha kampeni ya kufufua zao la michikichi ili kuweza kuzalisha mafuta ya kutosha.

Akizindua kampeni hiyo mkoani Kigoma hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kufanya mageuzi makubwa katika zao la michikichi.

Uamuzi huo sasa umelifanya zao hilo kuwa la sita la biashara ambalo katika miaka ya l960 hadi 1970, mkoa wa Kigoma ulijipatia umaarufu kwa uzalishaji wa zao hilo.

Waziri Mkuu anasema kampeni ya kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma inaenda sambamba na kuanzishwa kwa kituo cha utafiti wa zao hilo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga kilichopo wilayani Kigoma kwa kuwa ndiko zao la Michikichi linalimwa kwa wingi.

Anasema zao la mchikichiki ni muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa nchini, hivyo ufufuaji wa zao hilo ni kichocheo cha viwanda kwa kuwa kutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi na kuvutia wawekezaji.

Waziri Mkuu anabainisha kuwa licha ya kuwepo kwa michikichi mingi nchini lakini uzalishaji wake unafanyika kwa njia za kienyeji, hivyo Serikali imedhamiria kuboresha kilimo hicho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili liweze kuleta manufaa makubwa kwa Taifa na wakulima.


Hivyo makala ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI

yaani makala yote ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/zao-la-mchikichi-kumaliza-uhaba-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI"

Post a Comment