title : AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA
kiungo : AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA
AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora za Smartphone kupitia kitengo chake cha rasilimali watu wameandaa bonanza la michezo lililowashirikisha wafanyakazi wake wote kwa lengo la kujenga afya za wafanyakazi hao pamoja na kuongeza ushirikiano eneo la kazi.
Akiongea mara baada ya tamasha hilo kuisha Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu alisema “Airtel tunatambua jitihada za serikali zinazosisitiza kuboresha na kuweka mzingira rafiki sehemu za kazi, pia Airtel tunafahamu sana umuhimu wa michezo na mazoezi kwa afya za wafanyakazi wetu, Hivyo ndio maana tumeona ni vyema kukutana kwa michezo kama hivi ili kuwasaidia wafanyakazi kurelax na kubadilishana mawazo wakiwa katika mazingira tofauti”
Katika Bonaza hilo la muziki na mchezo wafanyakazi wengi walifurahia zaidi mchezo wa kupigiana penati ambao washiriki walikuwa ni wasichana wote kwa mgawanyo wa vitengo vyao vya kazi kikiwemo kitengo cha ofisi ya Mkurugenzi mkuu kinachoundwa na rasilimali watu na udhibiti huduma, kitengo cha masoko, huduma kwa wateja, kitengo cha mauzo, ununuzi na ugavi, pamoja na kitengo fedha na mipango.
katika mchezo huo ushiriki ulikuwa wenye uvutano mkubwa kwa mzunguko wa ngazi ya mtoano na kuwa wenye ushindani mkali zaidi pale ambapo walibaki vinara watatu ambao ni kitengo cha Huduma kwa wateja waliokichapa kitengo cha fedha na mipango kwa goli 6 huku wao wakiambuia goli tano na kuwafanya kitengo cha huduma kwa wateja kuibuka washindi wa ujumla na kubeba kombe la ushindi wa mchezo huo.
Mchezaji wa Kitengo cha Fedha cha Airtel Bi Foibe Simon akipiga penati dhidi ya kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa Bonanza la Familia ya wafanyakazi wa Airtel lililofanyika kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Meneja Rasilimali watu Pamela Mwandetele akipiga penati wakati wa bonanza Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Kushoto ni kocha wa timu ya kitengo cha fedha cha Airtel bw Sylivester Nsabi (Gadiola) na Nahodha wa timu hiyo Bi Foibe Saimon wakipokea kombe la ushindi wa pili toka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bw, Isack Nchunda wapilitoka kushoto akiwa na Mkurugenzi wa kitengo cha Fedha Bw Nishant Mohan. Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bw, Isack Nchunda akikabidhi zawadi ya kombe la mshindi wa pili kwa Nahodha wa timu ya kitengo cha Fedha na Mipango cha Airtel Bi Foibe Saimon mara baada ya kumalizika kwa bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (watatu toka kushoto) akikabidhi zawadi ya kombe kwa washindi wa kwanza ambao ni kitengo cha huduma kwa wateja walipoibuka washindi kwa kukiladha kitengo cha fedha na mipango kwa golo za penati 6-5 wakati wa Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki. Kitengo hicho pia watapata zawadi ya kwenye kupata chakula cha mchana kwenye hotel ya nyota tatu wote wakiwa wamelipiwa gharama zote na Airtel.
Wafanyakazi wa Airtel kitengo cha huduma kwa wateja wakishangilia na Kombe lao mara baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye bonanza la Airtel Familia lilifanyika mwishoni mwa wiki hii. Airtel imefanya bonanza hilo la lawafanyakazi ambapo wasichana toka vitengo mbalimbali ndani ya kampuni hiyo walishindani kupiga penati ambapo kitengo cha huduma kwa wateja waliibuka washindi kwa penati 6-5 dhidi ya kitengo cha Mipango na fedha cha Airtel.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA
yaani makala yote AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/airtel-ya-washiriki-bonanza-kujega-afya.html
0 Response to "AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA"
Post a Comment