title : WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU
kiungo : WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU
WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU
Na Jonas Kamaleki-MAELEZO, Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Andrew Massawe kusimamia ipasavyo mifuko mipya ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha michango ya watumishi inakusanywa.
Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kumpokea Katibu Mkuu huyo aliyeteuliwa hivi karibuni.“Katibu Mkuu nakuagiza uhakikishe michango inakusanywa na malipo yanalipwa kwa wakati ili kuondoa changamoto kwa wanufaika ikiwemo wastaafu”, alisema Mhagama.
Waziri Mhagama amemtaka Katibu Mkuu kusimamia vizuri uwekezaji uliofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii kabla ya kuunganishwa. Ametaja uwekezaji huo kuwa ni kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Magereza cha Karanga, Moshi, kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari cha Mkulazi.
Aidha, Waziri Mhagama amesema kiwanda cha sukari kitaongeza ajira hasa kwa vijana na kuongeza fedha za kigeni kwani uagizaji wa sukari toka nje utapungua.Kiwanda hicho kinatarajia kuzalisha tani 250 kwa mwaka, ambazo zikiunganishwa na uzalishaji wa viwanda vingine vya sukari nchini zitaondoa uhaba wa bidhaa hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu wa ofisi hiyo baada ya kumkaribisha rasmi ofisini hapo Agosti 3, 2018. (Katikati) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vina na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka ofisi hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alipowasili ofisini hapo Agosti 3, 2018 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa ofisi hiyo mara baada ya kukaribishwa rasmi ofisini hapo Agosti 3, 2018 Jijini Dodoma.
Hivyo makala WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU
yaani makala yote WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/waziri-mhagama-amkaribisha-rasmi-katibu.html
0 Response to "WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU"
Post a Comment