title : WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI
kiungo : WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI
WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wanafanya kongamano la kwanza na la kihistoria juu ya maendeleo mbalimbali yaliyotokea katika utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology) barani Afrika.
Kongamano hilo la siku nne linashirikisha nchi 15 za Afrika ikiwamo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Ivory coast, Swaziland, DRC, Madagascar, Ghana, Ethiopia pamoja na Burkinafaso
Akifungua kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Bakari Kambi amesema azma ya serikali ni kuendelea kuboresha huduma za afya nchini ili kuwawezesha Watanzania kupata matibabu ndani ya nchi .
‘’Miongoni mwa malengo makubwa ya serikali ya awamu ya tano ni kupanua wigo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi na kuhakikisha huduma za kibingwa na ubingwa wa juu zinatolewa hapa hapa nchini ili kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma hizo,’’ amesema Prof. Bakari.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema kukutana kwa watalaam hao ni hatua nzuri ya kuangalia namna bora ya kutoa tiba ya kisasa kwa magonjwa ya damu na hata kuanzisha tiba hiyo sehemu za kanda ili kupunguza idadi ya wagonjwa wengi ambao wanakuja kupata huduma hiyo Muhimbili.
“MHN tumekua wenyeji wa kongamano hili ambalo limehusisha wataalam wa magonjwa ya damu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, hii ni heshima kubwa na itasaidia kufikia malengo ya kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi,’’amesema Prof. Museru.
Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Bakari akizungumza na wataalamu wa magonjwa ya damu (Haematology) kwenye kongamano la kwanza ambalo limeandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza kwenye kongamano hilo baada ya kuwakaribisha wataalam wa magonjwa ya damu kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Wataalamu wa magonjwa ya damu kutoka nchi mbalimbali duniani wakifuatilia mkutano huo leo ambao unafanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Baadhi ya nchi zinazoshiriki kongamano hilo la siku nne ni Nigeria, Ghana, Bostwana, Afrika Kusini, Ufaransa, Marekani, Rwanda na Italia. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>
Hivyo makala WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI
yaani makala yote WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wataalam-magonjwa-ya-damu-kutoka-afrika.html
0 Response to "WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI"
Post a Comment