title : WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI
kiungo : WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI
WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Felix Lyaviva amewashauri wanafunzi waliopo shuleni kujiandaa kujiajiri na siyo kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao.
Lyaviva ametoa rai hiyo leo alipokuwa akifunga mafunzo ya ukakamavu ya wanafunzi wa Kidato cha Tano 2018 wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya jijini Dar es Salaam.
Akiwahutubia wanafunzi hao mbele ya wazazi, walimu, maafisa wa jeshi wakiwemo wastaafu na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, Lyaviva alisema; "Nawapongeza sana kwa mafunzo ya ukakamavu mliyopewa, mmeonesha ni jinsi gani mlivyoiva lakini niwaombe muwe na ndoto za kujiajiri siyo kuajiriwa mara mtakapotoka hapa."
Mkuu huyo wa wilaya, amewaasa wanafunzi kutojihusisha na vitendo vya mapenzi, uvutaji wa madawa ya kulevya na sigara ambavyo vinaathari kubwa katika maisha.
"Nyie wanafunzi wa kike, nawaasa msikubali kurubuniwa na wenzetu wa kiume kwani athari zake ni kupewa mimba ambazo zitawaharibia maisha yenu huku wao wakiendelea na masomo," alisema Lyaviva.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakifuatilia gwaride hilo.
Kikosi cha nne kikitoa heshima kwa mgeni rasmi kilipokuwa kikitembea kwa mwendo wa haraka.
Gwaride la ukakamavu likipita mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi zawadi Julieth Peter aliyekuwa kamanda wa kikosi namba tatu kwa kuongoza vizuri kikosi chake.
Hivyo makala WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI
yaani makala yote WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wanafunzi-kidato-cha-tano-2018.html





0 Response to "WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI"
Post a Comment