VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA

VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA
kiungo : VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA

soma pia


VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA

 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kulia) akizungumza na wazee wa eneo la makazi ya wazee, walemavu na watu wasio na uwezo leo jijini Dar es Salaam na kuwaambia vijana wanaoishi katika kambi hiyo waondoke mara moja.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kulia) akiteta jambo na mmoja wa maafisa ustawi wa jamii wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa kuwaondoa vijana hao katika kambi ya wazee Nunge iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri amewataka vijana waishio kwenye kambi ya wazee na wasiojiweza ya Nunge iliyopo Kigamboni kuondoka katika makazi hayo kama walivyopewa agizo hilo kuanzia Januari 4, 2016.

Akizungumza na vijana hao mara baada ya kutembelea kambi hiyo Msafiri ameeleza kuwa eneo la Nunge linatakiwa kuendelea kutumika kama ilivyopangwa yaani kuwa makazi ya wazee na wasiojiweza na kama Serikali wameandaa namna bora ya kuwaondoa vijana hao ambao wamekuwa wakiishi hapo baada ya kutolewa katika kambi ya watoto iliyopo Kurasini walipokuwa wakilelewa kama watoto yatima na waliokosa msaada.

Mkuu wa Wilaya amewataka vijana hao kuondoka kambini hapo leo na kabla ya kuondoka kila kijana atapewa kiasi cha shilingi laki moja kama kianzio.

Pia ameeleza kuwa vijana hao 34 wanaotakiwa kuondoka katika makazi hayo ni vijana 20 pekee walipokea fursa ya kupata mafunzo ya jeshi la mgambo ambayo serikali ya Wilaya ya Kigamboni iliitoa kwa vijana hao.

Aidha, Msafiri amewahaidi vijana hao waliotayari kupata mafunzo ya mgambo kwa gharama za Serikali akiwa Mkuu wa Wilaya atahakikisha vijana wote watakaohitimu watapata ajira za kudumu mahali popote nchini.

Akieleza historia ya vijana hao Afisa Ustawi Wilaya ya Kigamboni Ramadhani Yahya amesema kuwa vijana hao walitolewa katika kambi ya Kurasini na kuletwa kwenye makazi hayo yaliyotengwa kwa ajili ya wazee na wamekaa hapo kwa muda mrefu na kwa sasa wanatakiwa wakajitegemee ili kupisha makazi hayo kwa walengwa.

Pia amesema kuwa vijana wote wana wamevuka umri wa miaka 18 na wanajishughulisha na kazi mbalimbali hivyo wanaamini watamudu mahitaji yao.

Naye katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando amesema kuwa kuondoka kwao kambini hapo si kutengwa bali ni fursa ambayo itawasaidia katika kujijenga na kujitegemea ili kuweza kufikia malengo yao kama vijana wengine.

Kwa upande wao vijana hao wameishukuru Serikali kwa kuwapa makazi kwa muda huo na wameiomba wawaongezee muda ili waweze kujipanga zaidi kabla ya kuyaacha makazi hayo.


Hivyo makala VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA

yaani makala yote VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/vijana-waishio-kwenye-kambi-ya-wazee.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VIJANA WAISHIO KWENYE KAMBI YA WAZEE NUNGE WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA"

Post a Comment