UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI

UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI
kiungo : UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI

soma pia


UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI

Katibu mkuu wa UWT CCM, Queen Mlozi amesema Serikali imejitahidi kujenga miundombinu ya maji kwa ajili ya kuwawezesha akina mama kupata maji safi na salama,pamoja na ujenzi wa vituo vya afya umeendelea kuimarika ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Hayo ameyasema jana jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema, katika Sekta ya elimu pia Serikali imejitahidi kutoka bilioni 80 mpaka bilioni 300 ambapo sasa hata watoto wa kike wanapata fursa ya kusoma kwa kupata mikopo.

Amesema kuwa, wao kama UWT wanampongeza Rais Dkt, Magufuli kwa utekelezaji huu wa ilani ya Chama CCM,huku akiwasisitiza watoto wa kike kuzitumia fursa za elimu ambazo zinatolewa na Serikali ya awamu ya tano akiwata wajiepushe na mimba za utotoni ambazo zinawafanya wapoteze fursa za kupata elimu.

“Mpaka sasa zimetolewa bilioni 700 kwa ajili ya miradi ya maji ili kuhakikisha ile dhana ya kumtua mama ndoo kichwani inatekelezeka na lengo kubwa ni kuhakikisha UWT inasimamia serikali ya CCM kumkomboa mwanamke kiuchumi na kisiasa “amesema Mloz

Amesema kuwa,kuna vipaumbele vinne vya kubuni vyanzo vya mapato ya jumuiya, Kubainisha mali za UWT ili zitumike vizuri, Kuongeza idadi ya wanachama wa jumuiya, Tunawajengea uwezo viongozi mbalimbali ndani ya jumuiya ili waweze kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi.

“Tumefanikiwa kuhamisha wanawake wengi kujiunga na jumuiya yetu, tumeongeza wanawake kwenye nafasi za uteuzi katika sekta mbalimbali, huku ikiwa tumejipanga kupigania kupata dawati la jinsia ndani ya jeshi la polisi ili wanawake wanaopata matatizo waweze kuhudumiwa na kitengo hicho ” amesema Mlozi.

Hata hivyo, amesema wanamkakati wa kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba, ndani ya Halmashauri zetu mikopo kwa akina mama inatolewa bila riba na nasisitiza wakurugenzi watekeleze haya maelekezo bila urasimu wowote.

“Nawaomba wanawake wa Tanzania mjiunge katika vikundi vya ujasiriamali ili waweze kunufaika na hizi fursa za mikopo zinazotolewa na Serikali ya chama changu, kwa niaba ya wanawake wote naomba kumpongeza mwenyekiti wetu ambaye ni Rais katika kuendelea kuwateua wanawake katika nafasi mbalimbali katika serikali yake ” amesema mlozi

Aidha amesema, kuwa wanakwenda kuhakiki upya mali za jumuiya ya wanawake UWT. Inawezekana ule uhakiki uliofanyika na Dr. Bashiru ulikuwa wa haraka na sehemu nyingine kuna mali ziliachwa bila kuhakikiwa.


Katibu mkuu wa UWT CCM, Queen Mlozi
akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana Ofisi ndogo za CCM- Lumumba jijini Dar,
Mlozi amesema kuwa atahakikisha UWT inamkomboa mwanamke wa Kitanzania Kiuchumi kwa kumsaidia kupata mkopo pasipo kubagha kabila ,rangi ,dini wala kuangalia itikadi za kisiasa. 


Hivyo makala UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI

yaani makala yote UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/uwt-wampongeza-rais-dkt.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UWT WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,YASISITIZA WATOTO WA KIKE KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU ZITOLEWAZO NA SERIKALI"

Post a Comment