title : USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA
kiungo : USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA
USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA
Uanzishaji wa vyama vya umwagiliaji kwa ajili ya usimamizi wa skimu za umwagiliaji, ni suluhisho sahihi la utunzaji wa skimu hizo itakayoipelekea Tanzania kuwa ya viwanda kupitia kilimo cha Umwagiliaji.
Hayo yamelezwa leo Mjini Bariadi katika viwanja vya nane vya Nyakabindi na Bi Zukheri Huddi Afisa Maendeleo ya jamii kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alipokuwa akizungumza na wakulima, waandishi wa habari waliotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.Bi Zukheri amesema kuwa sheria ya Umwagiliaji namba 5 ya mwaka 2013 na kanuni zake za mwaka 2015 inahamasisha Skimu za umwagiliaji kusimamiwa na kuendelezwa na vyama vya umwagiliaji ili ziweze kuwa na ufanisi
Bi Zukheri ameeleza kuwa ili kilimo cha umwagiliaji kiwe endelevu na chenye tija kuweza kufikia Tanzania ya viwanda na Biashara wakulima wote nchini, wanaomiliki mashamba katika skimu za umwagiliaji wanatakiwa kujiunga katika vyama vya umwagiliaji jambo ambalo litasaidia wakulima kuweza kusimamia na kuihudumia miundombinu ya umwagiliaji ili iwe endelevu kwa kulipia ada za uendeshaji, matunzo na matumizi ya maji.
“Kuanzia tarehe ya kuanzishwa kwa chama cha umwagiliaji, katika skimu husika chama hicho kinatakiwa kusajiliwa chini ya sheria na kanuni za umwagiliaji, na wakulima wote watatakiwa kuwa wanachama wa chama cha umwagiiaji na watalazimika kutekeleza masharti ya chama hicho. “ Alisisitiza.
Bi Zukheri Aliendelea kusema kuwa, Sheria ya umwagiliaji na kanuni zake imeweka bayana kwamba, chama, taasisi au chombo chochote kinachojishughulisha na shughuli za umwagiliaji kama chama cha umwagiliaji kitatakiwa kutuma maombi yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kujaza form Nationa Irrigation Act no.2 ( NIA No. 2) ya maombi ya ukubalifu kisha kitapatiwa cheti cha ukubalifu na kitapaswa kuongozwa na sheria iliyowasajili (Certificate of Compliance ) cheti cha ukubalifu.
Maadhimisho ya siku ya wakulima nchini nanenane yanaendela katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu katika Mji mdogo wa Bariadi.
Katika Picha ni Mfano wa shamba la mpunga (kipando) katika moja ya eneo la mabanda yanayoshiriki maonyesho ya wakulima nanenane katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. (Habari na Picha na Kitengo cha Habari Tume ya Taifa ya Taifa ya Umwagiliaji)
Katika Picha Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Zukheri Huddi akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya nanenane vya Nyakabindi , Bariadi Mkoani Simiyu.
Bi Zukheri Huddi Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza kuhusu vyama vya umwagiliaji na Mkulima aliyetembelea Banda la hilo, katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Hivyo makala USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA
yaani makala yote USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/usimamizi-wa-skimu-za-umwagiliaji.html
0 Response to "USIMAMIZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUIJENGA TANZANIA YA VIWANDA"
Post a Comment