UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU

UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU
kiungo : UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU

soma pia


UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU


Na Magreth Kinabo, Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma amekitaka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya tafiti katika baadhi ya Sheria ambazo zinahitaji marekebisho ili kuweza kuongeza uzito wa mabadiliko hayo.

Mhe. Jaji Mkuu aliyasema hayo mapema Agosti 17, alipotembelewa na wajumbe wapya wa Baraza la Uongozi wa TAWLA, ambao waliongozwa na Mwenyekiti wao, Bi. Athanasia Soka na Mkurugenzi wa TAWLA, Bi. Tike Mwambipile, waliofika kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko hayo ya Sheria, Jaji Mkuu alisema yanawezekana kufanyika endapo utatifi wa kina utafanyika ili kuongeza uzito wa mabadiliko hayo, “ni vizuri unapotaka kufanya mabadiliko kisheria kufanya utafiti ,tunaweza kufanya kwa kushirikiana,” alisema Jaji Mkuu.

Awali akizungumzia kuhusu mabadiliko ya Sheria yanayohitajika, Mkurugenzi huyo wa TAWLA, Bi. Tike Mwambipile, aliitaja Sheria ya ndoa.

“Katika sheria hii mathalani kumekuwa na mgawanyo wa mali usio sawa hususani pale ambapo mwanaume inapothibitishwa ndiye anamiliki mali hupata asilimia nyingi na mwanamke hupata asilimia chache wakati ikithibitika mwanamke ndiye anamiliki mali hugawanywa asilimia 50 kwa asilimia 50,” alisema Bi. Mwambipile. 

Mhe. Jaji Mkuu akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa TAWLA, Bi. Athanasia Soka. 
Mhe. Jaji Mkuu akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Mwenyekiti wa TAWLA, Mhe. Jaji Mkuu pia amewapatia nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama. 
Mhe. Jaji Mkuu akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Mwenyekiti wa TAWLA, Mhe. Jaji Mkuu pia amewapatia nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama. 



Hivyo makala UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU

yaani makala yote UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/uongozi-mpya-wa-chama-cha-wanasheria.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE WAMTEMBELEA JAJI MKUU"

Post a Comment