TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA

TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA
kiungo : TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA

soma pia


TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Serikali imesema inafanya utaratibu wa kuwa na Hati ya Utambulisho wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana katika nchi ya Tanzania pekee katika vilima vya Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Agosti na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa Semina ya mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo imefanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.

Waziri Kairuki amesema kuwa, serikali inataka kuona kuwa dunia inafahamu kuwa, madini hayo yanapatikana Tanzania pekee na kuhakikisha kwamba yanajulikana zaidi.

Semina ya wabunge imefanyika kufuatia maelekezo ya Kamati hiyo ambayo ilitaka kufahamu kuhusu mwenendo mzima wa Madini ya tanzanite, biashara na udhibiti wa madini hayo baada ya kujengwa kwa Ukuta wa Mirerani unaozunguka migodi ya madini ya tanzanite, Muundo wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini na majukumu yao.

Waziri Kairuki amesema kuwa, Wizara imepata fursa ya kuwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwemo mikakati ya serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini hayo na mipango madhubuti ambayo serikali inakusudia kuifanya ili kuhakikisha kwamba rasilimali madini inalinufaisha taifa na hatimaye sekta ya madini iweze kufikia asilimia 10 ya machango wake katika pato la taifa ifikapo mwaka 2025.










Afisa Madini Mkazi wa Mirerani, Mhandisi David Ntalimwa, akieleza jambo wakati akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Nishati na Madini. 
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushauri na Uchambuzi wa Kazi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, akiwasilisha mada kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini. 
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizotolewa kwa kamati ya Bunge. 
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizotolewa kwa kamati ya Bunge. 



Hivyo makala TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA

yaani makala yote TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tanzanite-kuwa-na-hati-ya-utambulisho.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA"

Post a Comment