Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care)

Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care) - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care), tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care)
kiungo : Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care)

soma pia


Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care)

Na Salome Majaliwa 
Wafanyakazi kutoka kampuni ya Professional Cleaner ambao watakua wakitoa huduma kwa mteja (customer care) katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanya kazi kwa bidii kwa kutoa huduma bora kwa wateja ili kuboresha huduma za Taasisi hiyo. 
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa mafunzo mafupi kwa watua huduma hao leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. 
Prof. Janabi amesema katika kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Taasisi imeanzisha kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care) ili kupunguza msongamano wa foleni kwa wagonjwa wakati wa matibabu na kuongeza tija katika utoaji wa huduma. 
“Taasisi hii inaona wagonjwa wa nje kati ya 150 mpaka 300 kwa siku; ili Kuboresha huduma tunazozitoa Taasisi imeona ni vyema tuwe na kitengo cha huduma kwa mteja kitachoratibu utoaji wa huduma kwa wagonjwa kwa kufuata taratibu zilizopo” alisema Prof. Janabi 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Taasisi hiyo Agnes Kuhenga amewataka watumishi wa kitengo cha huduma kwa mteja kuwahudumia wagonjwa kwa kufuata haki na wajibu wa mtoa huduma kwa mteja. 
 Naye Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delila Kimambo amewahasa watumishi wa kitengo cha huduma kwa mteja kuwa na upendo kwa wagonjwa, kuwasikiliza na kuwajali pale wanapohitaji msaada kutoka kwao. 
“Wagonjwa hawafanani kuna wengine wanakuja wakihitaji huduma ya haraka zaidi; nyie mkawe msaada kwao kwa kuwa wabunifu ili huduma zinazohitajika ziweze kupatikana kwa wakati na kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa wetu” alisema Dkt. Delila
 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Taasisi hiyo Agnes Kuhenga

 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kutoa huduma bora kwa waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Idara ya Uuguzi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya (kulia) akitoa mada ya namna ya kupokea wagonjwa kwa waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi wa kampuni ya Professional Cleaner ambaye ni mmoja kati ya watoa huduma kwa mteja (customer care) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Khadija Abeid akielezea namna ambavyo atakua akitoa huduma bora kwa wateja wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu


Hivyo makala Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care)

yaani makala yote Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/taasisi-ya-moyo-yaanzisha-kitengo-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Taasisi ya Moyo yaanzisha Kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care)"

Post a Comment