title : SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA.
kiungo : SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA.
SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatarajia kufanya udahili wa wanafunzi kwa asilimia 100 kutoka wanafunzi Mia moja na Hamsini (150) hadi Mia tatu themanini wa kada za Afya nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga, yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na MALARIA (Global fund).
Waziri ummy aliendelea kusema kuwa majengo yaliyokabidhiwa ni juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha wanazalisha wataalamu wa kada za Afya, hususani Wauguzi na Wakunga jambo litalowawezesha kuwa Wataalamu bora.
“Udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka 190 hadi 260, Huwa tunapata shida sana, wanafunzi wengi wanafaulu na tunakuwa hatuna nafasi ya wapi pakuwapeleka, kwahiyo tunawashukuru Global fund , tunaweza kudahili hadi wanafunzi 368” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya kushirikiana na NACTE kuwachukua wanafunzi wote waliosoma na kufaulu vizuri masomo nya Sayansi na wenye vigezo na wenye vigezo katika kada ya Afya.
Waziri Ummy aliongeza kuwa, kutokana na jitihada hizo kumekuwepo na ongezeko la wahitimu ngazi ya astashahada na Stashahada kwa mafunzo kutoka wahitimu 4473 mwaka 2012/2013 hadi 7561 kwa mwaka 2016/2017 , ongezeko hili ni sawa na Asilimia 69.
Wakati huo huo Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle amesema kwa mwaka huu wa fedha , Wizara imetenga shilingi Bilion 8 kwaajili ya ukarabati wa majengo chakavu katika chuo hicho.
Amesema kuwa Wakufunzi 143 wamepangiwa kufanya kazi katika vyuo vya Afya nchini, vikiwemo vyuo vya Wauguzi na Wakunga ambao ndio msingi wa kupunguza athari ya uzazi pamoja na vifo vya wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Mwakilishi wa Global Fund Dkt. Eltrudis Temba amesema kuwa, Global fund imeboresha miundombinu yakufundishia katika vyuo 14 na kuwezesha kufadhili zaidi ya wanafunzi 1500 wa kada za Uuguzi na Ukunga wa Technolojia dawa, Technolojia maabara na Tabibu katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018, pamoja na kutenga shilingi Billion 1.1 kwaajili yakuboresha mifumo ya Afya.
Hivyo makala SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA.
yaani makala yote SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/serikali-kudahili-wanafunzi-380-sekta.html
0 Response to "SERIKALI KUDAHILI WANAFUNZI 380 SEKTA YA AFYA."
Post a Comment