RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR

RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR
kiungo : RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR

soma pia


RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR


*Ataka yalipiwe kodi kwa mujibu wa sharia, aonya 
*Asema sheria za kodi ni mtu mmoja tu ndio amepewa dhamana 
*Abaini ujanja ujanja, ataka wafanyakazi wasitumike 



Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
RAIS Dk.John Magufuli ameamua kuvunja ukimya kwa kuamua kuzungumzia suala la makontena ambayo yameletwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. 

Amesema makontena hayo lazima yalipwe kodi na kuwataka viongozi wa ngazi zote kokote walipo kuhakikisha wanajenga utamaduni wa kuwatumikia Watanzania na si kufanya kazi kwa kuwatumikia watu fulani. 

Rais Dk.Magufuli akizungumza leo mkoani Chato ameamua kuzungumzia suala hilo la makontena ya Makonda na ambapo amesema eti kuna Mkuu wa Mkoa(hakumtaja jina) ameleta makontena na ameambiwa alipe kodi na kuhoji kwanini asilipe kodi. 

Amesema kuwa katika sharia za nchi ni kwamba sharia namba 30 ya mwaka 1974 ya sharia ya fedha, sharia ya madeni na misaada ni mtu mmoja tu ndio anahusika na masuala ya msamaha. 

“Kupitia sharia namba 30 ya mwaka 1974 nafikiri kifungu cha 3, 4 na 5 ndio kinatoa mamlaka kwa anayehusika katika hilo na hakuna mtu mwingine yeyote,”amefafanua. 

Rais Dk.Magufuli amesema “Sasa ukichukua makontena kule, umezungumza na watu wengine labda wafanyabiashara unasema una makontena yako.Halafu unasema ni ya walimu wakati hata shule hazitajwi 

“Maana yake unataka kuchukua machache na kisha uyapeleke kwenye shule mbili au tatu na yaliyobakia ufanye biashara kwa kuyapeleka kwenye ‘Shoping Mall’, kwani walimu wamesema wanataka masofa wakalale?. 

Kabla ya kauli ya Rais Magufuli ambayo ameitoa leo mkoani Chato, Jumatatu ya wiki hii Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango alishatoa msimamo wake kwamba lazima makontena hayo yalipiwe kodi na ikishindikana yapigwe mnada. 



Dk.Mpango akaenda mbali zaidi kwa kusema anashangazwa na namna ambavyo jambo hilo linazungumzwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii lakini amekaa kimya kwasababu hana tabia ya kuzozana. 

Dk.Mpango alisema kuwa lazima sharia ichukue mkondo wake na yeye amepewa dhamana ya kusimamia. Akatoa tahadhari kwa viongozi kuwa makini na kauli zao. 

Alisema inashangaza kusikia Mkuu wa Mkoa akisema atakayenunua samani zilizopo kwenye makontena hayo atapata laana ambapo akafafanua hakuna laana yeyoye na kuwataka watu wayanunue baada ya TRA kutangaza mnada. 

Wakati Makonda anazungumzia Makontena akiwa kanisani wilayani Ngara mkoani Kagera aliamua kuelezea namna ambavyo baadhi ya watu wanakwamisha kutolewa kwa makontena hayo na kwenye orodha hiyo na alimtaja Waziri wa Fedha. 

Makonda akasema kuwa watakaonunua makontena hayo watapaata lakini huku akieleza wazi iwapo wataendelea kukwamisha atamwambia Rais. 


Hivyo makala RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR

yaani makala yote RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/rais-magufuli-atoa-msimamo-makontena-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR"

Post a Comment