title : NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2
kiungo : NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2
NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo matatu na wa udiwani katika kata mbili za Tanzania Bara utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu.
Akitangaza uchaguiz huo mjini Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk alisema fomu za uteuzi wa wagombea wa Majimbo hayo zitatolewa kuanzia tarehe 13 hadi 20 Agosti, mwaka huu na uteuzi utafanyika tarehe 20 Agosti, 2018 wakati kampeni zitaanza zitaanza tarehe 21 Agosti, na kumalizika tarehe 15 Septemba, mwaka huu.
Jaji Mbarouk alisema “Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo matatu”
Aliyataja majimbo hayo kuwa ni Korogwe Vijijini, Mkoa wa Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndugu Stephen Hilary Ngonyani, Jimbo la Ukonga Katika Mkoa wa Dar Es Salaam na Jimbo la Monduli katika Mkoa wa Arusha .Alisema wabunge wa majimbo hayo mawili Ndugu Mwita Mwikabe Waitara na Ndugu Julius Kalanga Laizer wajiuzulu uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hivyo kupoteza sifa za kuwa Wabunge.
“Baada ya kupokea taarifa hizo na kwa mujibu wa vifungu vya 37 (1) (b) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa taarifa kwa Umma kuwa majimbo matatu ya Korogwe Vijijini, Ukonga na Monduli yapo wazi”, alisema. Katika hatua nyingine, Jaji Mbarouk alisema kwa kuzingatia masharti ya vifungu vya 37(1)(b) (5) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume inatoa taarifa wa Umma kuhusu Ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo hayo.
Hivyo makala NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2
yaani makala yote NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/nec-yatangaza-uchaguzi-mdogo-wa-ubunge.html
0 Response to "NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2"
Post a Comment