title : NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU
kiungo : NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU
NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WATU nane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kuongoza mbinu za kiuhalifu na kusaidia kusafirisha binadamu.
Hata hivyo, ni watuhumiwa wanne tu waliofanikiwa kusomewa mashtaka yao kwa kuwa watuhumiwa wengine wanne hawakuwa wakijua kiswahili wala kiingereza.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali, Faraji Nguka amewataja washtakiwa wanne waliosomewa mashtaka yao kuwa ni, Abdallah Kassim Bashrahil, Idd Hussein Said, Muhidin Said Machelenga, Swed Twaibu Swed.
Mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde imedaiwa kuwa, katika siku na mahali tofauti tofauti, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, na nchi ya Comorro washtakiwa hao waliongoza genge la uhalifu na kuweza kutekeleza tukio la kusafirisha binadamu kutoka Comorro kwenda Saudi Arabia kupitia Tanzania.
Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa hao, walisaidia kuwasafirisha Halima Mmadi, Tereha Mlahaili, Ali Miraaji na raia 162 huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Imedaiwa kuwa walifanya hivyo kwa kuwapatia hati za kusafiria za Tanzania huku wakijua kuwa watu hao ni raia wa Commoro.
Pia washtakiwa wanadaiwa kufanya hivyo ili kuwarahisishia kupata kibali cha makazi kutoka Idara ya Uhamiaji ya Tanzania kwa lengo la kuwasafirisha watu hao kwenda nchini Saudi Arabia.
Hats hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi mahakama kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 27, 2018 kwa ajili ya washtakiwa wengine wanne kusomewa mashtaka yao mkalimani atakapopatikana
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika.
Watuhumiwa wanaotarajiwa kusomewa mashtaka yao Siku ya Jumatatu ni, Said Ally, Ahamada Mchangama, Hamada Ali Ben Ali na Suulaimana Abdallah.
Hivyo makala NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU
yaani makala yote NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/nane-wafikishwa-mahakama-ya-kisutu-kwa.html
0 Response to "NANE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHARIFU"
Post a Comment