title : Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa
kiungo : Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa
Na.Is-haka Omar. Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi amesema
taasisi hiyo inathamini juhudi na mchango wa kuwasadia
watoto yatima zinazofanywa na wadau wa maendeleo kutoka
nchi mbali mbali duniani.
Hayo aliyasema wakati alipotembelea Kituo cha kulelea
watoto yatima kinachomilikiwa na shirika la Direct AID
kutoka nchini Kuwait kilichopo mtaa wa Ijitimai ya zamani
Mwanakwerekwe Unguja, Dk. Mabodi alieleza kuwa
ameridhishwa na juhudi za kituo kinachowapatia malezi
bora watoto yatima wanaolelewa na shirika hilo.
Alisema shirika hilo limekuwa likifanya kazi kubwa ya
kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala
ya kijamii hasa uimarishaji wa huduma za maji safi na
salama na elimu.
Dk.Mabodi alisema kwamba CCM ikiwa ni taasisi ya kisiasa
itaendelea kuwa karibu na mashirika mbali mbali yenye
dhamira ya kuendelea kuunga mkono juhudi za
serikali, katika kutatua kero na changamoto za jamii.
Amefafanua kwamba watoto ambao wazazi wao wamefariki
wasipotunzwa na kuhudimiwa vizuri wanaweza kukosa haki
zao za msingi zikiwemo malezi mazuri na elimu bora.
Alitoa wito kwa wananchi wa maeneo mbali mbali kuwa
karibu na Watoto yatima kwani wengi wao wanakuwa
wakitengwa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishwaji hata
kukosa fursa ya kupewa huduma muhimu za kibinadamu.
“CCM tutakuwa karibu zaidi na Direct AID kwani mmeamua
kuisaidia jamii yetu nasi lazima tuonyeshe ungwana wetu wa
kushirikiana nanyi kutatua changamoto zinazowakabili
katika upangaji wa mikakati yenu ya kuisaidia jamii.”,
alisema Dk. Mabodi.
Naye Mkurugenzi wa shirika hilo, Nd. Ayman Mohamed
alisema shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kuwapatia
elimu watoto hao ili waweze kuwa na uwezo wa kujitegemea
wenyewe mara baada ya kumaliza muda wa kuishi katika
kituo hicho.
Alisema kituo hicho kimeweza kutoa vijana wengi wasomi
wanaofanya kazi katika sekta mbali mbali za serikali na
binafsi.
Nd.Ayman aliyataja malengo ya shirika hilo kuwa ni kujenga
Vituo vya kisasa vya kulelea watoto yatima vitakavyokuwa na
shule, vituo vya Afya na vyuo vya masomo ya dini ya
kiislamu kwa Unguja na Pemba.
Akizungumza mmoja ya vijana waliolelewa katika Kituo
hicho, Mhandisi Abdulahi Salum Kassim alisema kituo
hicho kimemlea akiwa na umri mdogo na kumsomesha hadi
ngazi ya elimu ya juu ambapo hivi sasa ni mtumishi
serikalini.
Alikiri kuwa mafanikio hayo yametokana na utaratibu mzuri
uliowekwa na serikali wa kuruhusu shirika la Direct AID
kuwasaidia watoto yatima.
“Shirika hili limenilea nikiwa mtoto mdogo na kunisomesha
mpaka nimekuwa mtu mzima mwenye familia ambaye pia
nawasaidia vijana wenzangu ambao nao wazazi wao
walifariki wakiwa wadogo.”, alifafanua Mhandisi Abdulahi.
Naye Diwani wa Wadi ya Meli nne, Saleh Juma Kinana
ambaye pia ni miongoni mwa vijana waliolelewa katika Kituo
hicho, alisema watoto yatima wanatakiwa kulelewa na
kuthaminiwa kama walivyo watoto wengine katika jamii.
Kituo hicho kinafuata malezi na miongozo ya dini ya Kiislam
kina jumla ya watoto 44 ambao ni watoto yatima.
Hivyo makala Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa
yaani makala yote Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/naibu-katibu-mkuu-wa-ccm-zanzibar-ndg.html
0 Response to "Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Abdalla Juma Mabodi Amesema Watoto Yatima Kuthaminiwa"
Post a Comment