MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA

MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA
kiungo : MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA

soma pia


MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza washindi wa Multichoice Talent Factory watakaoenda kupata mafunzo ya mwaka mmoja Nchini Kenya.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo akiwa pamoja na washindo wa shindano la Multichoice Talent Factory watakaoenda kupata mafunzo ya mwaka mmoja nchini Kenya.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania imetawatangaza vijana wanne wa ktanzania waliofanikiwa kushinda shindano la Multichoice Talent Factory watakaoungana na wenzao kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kwa ajili ya kupata mafunzo ya filamu kwenye vituo vitatu tofauti.

Washindi hao waliofanikiwa kushinda wataelekea nchini Kenya kwa ajili ya mafunzo hayo yatakayokuwa ya mwaka mmoja yakianzia Oktoba Mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa mchakato mzima wa kuwapata washindi hao ulichukua muda wa miezi miwili baada ya kuzinduliwa mwezi Mei mwaka huu, na zaidi ya vija a 160 walituma maombi na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai na kuwapata vijana hawa walioshinda.

Shelukindo amesema kuwa, maendeleo ya nchi kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi zilizopo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori huku sekta ya sanaa na ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo kupelekea mchango mdogo kwenye ukuaji wa uchumi.

Amesema kuwa ili kuhakikisha wanasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya wahimili wa uchumi wa nchi , Multichoice imeweza kuanzisha program hizo na wameanza na sekta ya filamu na tayari wameshapatikana vijana hao watakaoanza mafunzo mwezi Oktoba nchini Kenya.

Shelukindo amewataja  vijana hao ni Sarah Kimario kutoka Dar es Salaam, Wilson Nkya wa Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi wa Kilimanjaro na safari yao tayari imeshapangwa wanasubiriwa kusafiri tu.

Mmoja wa washindi waliotangazwa kufuzu program Sarah Kimario amesema kuwa hii ni moja ya nafasi nzuri ya kuweza kujifunza zaidi  masuala ya sanaa na amewaomba wazazi kutokuwakataza watoto wao kufanya kile wakipendacho kwani watakuwa wanashindwa kuonyesha vipaji walivyonavyo.


Hivyo makala MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA

yaani makala yote MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/multichoice-yawapa-fursa-ya-mafunzo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA"

Post a Comment