Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI

Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI
kiungo : Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI

soma pia


Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI

Na Andrew Chale
Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh, Abu Bakari Zuberi  leo Agosti 31,2018 amemtembea na kumuombea dua maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara. 

Mufti, Sheikh Zuberi  aliambata na Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA, Sheikh  Yusuph Hassan Tonge ambapo kwa pamoja wameweza kuendesha dua maalum ili kupona haraka majeraha yake.

“Nimetoka Makka kwenye hijja tumekuombea dua. Nimerejea nikaona nije kukuona na pia kukuombea dua ili upone haraka.”  Alisema Mufti, Sheikh Zuberi.

Mbali na dua, pia Mufti, Sheikh Zuberi ameweza kumpongeza Dkt. Kigwangalla kwa juhudi zake za kazi katika Wizara yake hiyo.

Aidha, Dkt. Hamisi Kigwangalla amemshukuru Mufti Mkuu, Sheikh Zuberi  pamoja na BAKWATA kwa kuendelea kumuombea dua ambapo pia aliwaeleza kuwa kwa sasa hali yake inazidi kuimarika huku akisubiria ripoti za Madaktari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Taasisi ya MOI, Fiderisi Minja ambaye aliwapokea wageni hao, amesema kuwa Madaktari Bingwa na Wauguzi wanaendelea kutoa tiba bora  kwa wagonjwa wote wanaofika kufanyiwa tiba katika taasisi hiyo.

Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.


Hivyo makala Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI

yaani makala yote Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mufti-mkuu-sheikh-abubakar-zuberi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mufti Mkuu, Sheikh Abubakar Zuberi amfanyia dua Dkt. Kigwangalla MOI"

Post a Comment