title : Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote
kiungo : Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amewaahidi watumishi wa halmashauri ya Meru kuwapa ushirikiano wa kuweza kutimiza majukumu yao ikiwa ni njia mojawapo ya kutoa huduma bora kwa wananchi .
Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi, watumishi wa halmashauri hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambapo aliwahaidi kuwapa ushirikiano watumishi wote katika swala zima la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
"Napenda kuwatoa hofu watumishi wote kwa ujio wangu kwani nitawapa ushirikiano na kuwawezesha kutimiza majukumu yenu ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma bora ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi pamoja na rasilimali za Tanzania ili kuwanufaisha wananchi wote hasa wanyonge na watoto wa maskini, nukuu nimekuja hapa kutimiza torati na si kuivunja" alisema Mhe. Muro.
Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaanza kwa kuwapa fursa watumishi hao kwa kueleza changamoto zao na kupokea mawazo,maoni na mikakati itakayoleta maendeleo kwenye halmashauri hiyo na Wilaya ya Arumeru. Alibainisha kuwa anatarajia kufanya kikao kingine Jumatatu Agosti 6 2018.
Awali aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta akimkabidhi ofisi hiyo alisema kuwa watumishi wa Meru ni wazuri na wachapakazi na amemkabidhi pamoja na ofisi wakiwa weupe na wenye afya tele pia wanyeyekevu.
Mhe. Kimanta aliwawataka watumishi hao kumpa ushirikiano mkubwa mkuu huo mpya wa wilaya kama walivyompa yeye ili kuweza kuwaletea maendeleo wananchi wa meru na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru akiongea kabla ya kukabidhi ofisi kwa DC mpya Mhe. Jerry Muro.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru wakiwa kwenye kikao hico
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akiongea kwenye kikao hicho
Hivyo makala Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote
yaani makala yote Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkuu-mpya-wa-wilaya-ya-arumeru-mhe.html
0 Response to "Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote"
Post a Comment