mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil.

mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil.
kiungo : mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil.

soma pia


mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil.




Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja ya kuendelezwa kwa Kamisheni ya pamoja kati ya Tanzania na Brazil itakayoratibu mashirikiano ya Kidiplomasia katika Nyanja za Kiuchumi, Historia na Maendeleo ikilenga kuimarisha ustawi wa Wananchi wa pande hizo mbili .
Alisema Tanzania na Brazil pia zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni na Biashara unaopaswa kuendelezwa  kwa kuzingatia  kwamba ni Mataifa yanayofafana Kimaendeleo katika harakazi zao za kujiimarisha Kiuchumi.
Akizungumza na Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC}  Ofisini kwake Vuga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Kamisheni ya pamoja kati ya pande hizo mbili ipo lakini kinachohitajika kwa sasa ni ufuatiliaji wa malengo iliyoazimia kuyatekeleza.
Balozi Seif alisema Zanzibar kwa upande wake inaweza kufaidika  na mpango huo kwa kujikita zaidi katika kufungua milango ya Ushirikiano na Nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kwenye Sekta za Biashara, Taaluma katika masuala ya kukabiliana na Maafa pamoja na huduma za Afya.
Aliueleza ujumbe huo wa Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC} ikiongozwa na Bwana Fabio Webber Tagliari  kwamba  Zanzibar hivi sasa inaendelea kuimarisha Sekta ya Afya kwa kuvijengea uwezo zaidi vitengo vinavyosimamia huduma za  Afya ya Mama na Mtoto.
Balozi Seif alifahamisha kwamba uamuzi wa  Taasisi hiyo  ya ABC kutoka Brazil ya kufanya ziara ya kuangalia uwajibikaji katika Sekta ya Afya Zanzibar  unakwenda sambamba na azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ya kuimarisha  huduma za Afya  katika umbali usiozidi Kilomita Tano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein Nchini Brazil katika kipindi kilichopita  imeanza kuleta faida kutokana na Nchi hiyo kushawishika na hatimae kuamua kufungua Ubalozi wake Mdogo Visiwani Zanzibar.
Alisema kwa hatua hiyo yenye muelekeo wa kukomaa kwa uhusiano wa pande hizo mbili milango ya Zanzibar iko wazi kwa Taasisi na Makampuni ya Brazil kuweza kuanzisha miradi yao ya Uwekezaji Zanzibar kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya Sekta ya Utalii.
Alieleza kwamba Brazil tayari imeshapiga hatua kubwa katika uendeshaji wa Sekta hiyo ya Utalii kiasi kwamba Taasisi  na Makampuni yake yanaweza kutanua Wigo wao wa Uwekezaji zaidi katika kulitumia soko la Zanzibar linalokamilisha Ujenzi wa Maegesho ya Ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Aman Karume Zanzibar .
Naye kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC} Bwana Fabio Webber Tagliari alisema Taasisi yao imeweka upendeleo Maalum wa kusaidia kutoa huduma za Afya Visiwani Zanzibar.
Bwana Fabio Webber alisema Wataalamu wake wamepanga kutembelea baadhi ya Hospitali na Vituo vya Afya kuona changamoto zilizomo na kuangalia namna Taasisi yao inavyoweza kusaidia nguvu za Kitaalamu katika Utoaji wa huduma za Afya ikiwemo Upasuaji.
Alisema Wataalamu na Madaktari hao wanafurahia  kuungana pamoja na Wataalamu pamoja na Madaktari Wazalendo katika kutoa huduma za Afya kwa Wananchi mbali mbali.


Hivyo makala mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil.

yaani makala yote mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar-mhe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil."

Post a Comment