title : KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA
kiungo : KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA
KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA
Benny Mwaipaja, MOFP, Dar es Salaam
KATIBU MKUU wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amewaonya watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA wanaojihusisha na vitendo vya ukosefu wa maadili vinavyochangia kuikosesha serikali mapato yake yatokanayo na kodi, vikiwemo vitendo vya rushwa, kwamba watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
Bw. James, ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha kikao maalum kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Menejimenti pamoja na Mameneja wa Mikoa yote ya Tanzania Bara wa Mamlaka hiyo.
Amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo ikiwemo vitisho kwa wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi havikubaliki na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kukabiliana navyo kwa nguvu zote.Tayari wafanyakazi kadhaa wa Mamlaka hiyo wamefukuzwa kazi huku wengine wakihamishwa vituo vyao vya kazi kutokana na mwenendo wao usioridhisha na kulalamikiwa kutofuata maadili yao ya kazi wakati wanatekeleza majukumu yao.
Katibu Mkuu huyo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kuhakikisha kuwa inafikia malengo ya kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 18 katika mwaka huu wa Fedha wa 2018/2019, ikiwa ni sehemu ya Bajeti ya shilingi trilioni 32.47, iliyopitishwa na Bunge ili kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo.
Kwa Upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bw. Adolf Ndunguru, amesema kuwa Mamlaka yake imefanyakazi kubwa ya kuongeza makusanyo ya kodi kutoka wastani wa shilingi bilioni 800 hadi kufikia shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi.
Bw. Ndunguru amebainisha kuwa mafanikio mengine ni pamoja na kuongeza idadi ya walipakodi ikiwemo kuwasajili na kuwarasimisha wafanyabiashara ndogondogo walioko katika sekta isiyo rasmi ili waweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
Ametaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Mamlaka yake kuwa ni upungufu wa wafanyakazi, vitendeakazi yakiwemo magari, matumizi madogo ya mashine za EFD na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo kukwepa kodi, jambo ambalo amesema wameanza kulikabili na hatua zake zimeanza kuzaa matunda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini-TRA, kuweka mikakati ya namna Mamlaka hiyo inavyoweza kufanikisha ukusanyaji wa shilingi trilioni 18 ambazo Serikali imeipangia kukusanya katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi, (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Uhusiano wa Sekta Binafsi na Serikali (PPP), Dkt. John Mboya, wakifuatilia mkutano kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila (kushoto) na Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama ya Kitaifa, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, wakiwa katika Mkutano maalum kati ya Manejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA-kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, uliofanyika Jijini Dar es Salaam uliojadili fursa na changamoto za kufikia malengo waliyopangiwa TRA ya ukusanyaji kodi, Shilingi trilioni 18, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Kaimu Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Mgonya Benedicto (kulia), akiwa katika Mkutano maalum kati ya Manejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA-kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, uliofanyika Jijini Dar es Salaam, uliojadili fursa na changamoto za kufikia malengo waliyopangiwa TRA ya ukusanyaji kodi, Shilingi trilioni 18, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, mkoa wa Kilimanjaro, Bw. MMsafiri Mbibo, akichangia hoja wakati wa kikao maalum kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kuweka mikakati ya namna Mamlaka hiyo inavyoweza kufanikisha ukusanyaji wa shilingi trilioni 18 ambazo Serikali imeipangia kukusanya katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Hivyo makala KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA
yaani makala yote KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/katibu-mkuu-hazina-doto-james.html
0 Response to "KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA"
Post a Comment