title : MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA.
kiungo : MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA.
MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA.
Katibu tawala wa Manispaa ya Kigamboni Rahel Mhandao, akitangaza matokeo ya nauchaguzi wa Naibu meya wa Halmashauri hiyo kulia ni Meya wa wa manspaa hiyo Maabadi Hoja katikati ni kaimu Mkurugengenzi wa kigamboni David sukali.
Diwani wa viti maalumu Zuhura Dolla CCM akipiga kura ya katika uchaguzi wa naibu meya wa Manispaa ya Kigamboni .
Mwamba wa habari
Na John Luhende
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na mshindi wa kishindo katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam ambapo mgombea wake Diwani wa Kata ya Kibada, Amin Mzuri Sambo , amepata kura nane kati ya tisa zilizopigwa.
Katika uchaguzi huo, uliofanyika leo jioni, Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye ni Diwani wa Kata ya Tungi, Ernest Mafimbo, alijitoa katika dakika za mwisho na kushangaza wajumbe kuwa hakuwa na taarifa kwamba anagombea.
“Mimi sikuwa na taarifa kwamba nagombea. Chama cha wananchi CUF hakijanipa barua ya kuteuliwa kushiriki uchaguzi huu.
Ndiyo maana hata hapa hawapo,”alisema Mafimbo, hali iliyozua hali ya sitofahamu ukumbini.
Hata hivyo Ofisa wa Uchaguzi huo Magdalena Malunda aliwathibitishia wajumbe kuwa, Halmshauri iliviandikia vyama vyote vyenye madiwani katika baraza hilo na kwamba CUF ilimtambulisha Mafimbo kwa barua kuwa ndiye mgombea hivyo inashangaa kusikia akisema hana taarifa.
Kufuatia hali hiyo Mafimbo alitangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho hivyo kumpa upenyo Mzurisambo kuwa mgombea pekee.
Akitangaza matokeo mara baada ya upigaji kura kukamilika, Katibu Tawala wa Hal,shauri ya Manispaa ya Kigamboni, Rachael Mhando alisema, kura zilizopigwa zilikuwa tisa ambapo kura moja ilikuwa ni ya hapana hivyo kumtangaza Mzurisambo kuwa Naibu Meya.
Mzurisambo ambaye alikuwa akitetea kiti hicho ambacho amekiongoza tangu mwaka 2016, aliwashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuongoza tena na kwamba atashirikiana kwa karibu na viongozi na wananchi wa Kigamboni katika kuieletea maendeleo wilaya hiyo.
Mbali na uchaguzi huo wa Naibu Meya ambao hufanyika kila mwaka, pia baraza hilo lilifanya uchaguzi wa wenye viti wa kamato mbalimbali.
Hivyo makala MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA.
yaani makala yote MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mgombea-wa-cuf-nafasi-ya-naibumeya.html
0 Response to "MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA."
Post a Comment