MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI

MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI
kiungo : MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI

soma pia


MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI

Na Lucas Mboje, Magereza;

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Maofisa na askari wa Jeshi hilo kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kazi yao, badala yake wazingatie kanuni, miiko na maadili ya uendeshaji wa Jeshi la Magereza.

Kamishna Jenerali Kasike ametoa rai hiyo jana Agosti 1, 2018 wakati akiongea na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Arusha alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo.Alisema kuna upungufu katika uzingatiaji wa maadili kwa baadhi ya Maofisa na askari hususani mahusiano mabaya ya askari na wafungwa ikiwemo tabia za askari kuingiza simu magerezani.

Amesema hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa maofisa na askari watakaobainika kufanya vitendo hivyo ikiwemo kuwajibishwa na kufukuzwa kazi."Mnajua kabsaa gharama za kujihusisha na tabia hizi za mahusiano mabaya na wafungwa nawaasa mzingatie maadili mnapotekeleza majukumu yenu ya kazi". Alisisitiza Kamishna Jenerali Kasike. 

Kuhusu agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa Kamishna Jenerali Kasike amesena kwa sasa Jeshi hilo linakamilisha mpango kazi wake utakaowezesha utekelezaji wa agizo hilo.Amewataka askari wote nchini kujiandaa kisaikolojia kutekeleza agizo hilo bila kisingizio chochote kwani Jeshi la Magereza linazo rasilimali za kutosha kutekeleza agizo hilo.

"Tunayo ardhi yakutosha, nguvu kazi ya wafungwa ipo hivyo agizo la Rais na Amiri Jeshi Mkuu lazima litekelezwe bila kisingizio chochote". Alisema Jenerali Kasike.Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Arusha ambapo lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kuzungumza na Maofisa na askari wa Jeshi hilo.


Hivyo makala MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI

yaani makala yote MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/maofisa-wa-jeshi-la-magereza-waaswa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI"

Post a Comment