MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF

MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF
kiungo : MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF

soma pia


MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF

*Ni kwa ajili ya kilelezo katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF,wenzake.

Na mwandishi wetu, Glogu ya Jamii
MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea nyaraka ya kanuni za Fedha za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kama kielelezo cha ushahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake wanne.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametolewa uamuzi huo, leo baada ya kupitia hoja za pingamizi za kielelezo hicho, zilizowasilishwa ba Wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza na zile za upande wa Jamuhuri.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri amesema si sahihi kusema nyaraka ya kanuni za fedha za TFF iliyowasilishwa mahakamani hapo imetengenezwa, 
 kwani hiyo ni nyaraka ya umma,  na chini ya sheria ya ushahidi haihitaji uthibitisho wa kisheria.

Hivyi amesema inakubalika na imepokelewa kama kielelezo cha ushahidi.

Uamuzi huo, umetolewa baada ya Katibu Mkuu wa (TFF), Kidao Wilfred wakati akiongozwa na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kutoa ushahidi katika kesi hiyo, kudai kuwa TFF katika kukopa fedha inaongozwa na Kanuni za Fedha za TFF na katiba ya shirikisho hilo ya mwaka 2013 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2015.

Baada ya kueleza hayo, shahidi huyo aliomba mahakama ipokee katiba ya TFF na kanuni za fedha za shirikisho hilo kama kielelezo cha ushahidi kwenye kesi hiyo.

Wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza na Abraham Senguji walipinga kupokelewa kwa nyaraka hiyo ya kanuni za fedha za TFF kwa madai ya kwamba nyaraka hiyo ni nakala na siyo halisi na kwamba imekuwa kama ya kutengeneza.

 Baada ya uamuzi huo kutolewa, Wakili Swai aalidai hawana shahidi kwani Shahidi Kidao ambaye alitarajiwa kuendelee kutoa ushahidi amepata udhuru kwa sababu wamepata ugeni kutoka CECAFA,  hivyo anahusika sehemu kubwa katika ugeni huo.

Kesi hiyo imeiahirishwa hadi Septemba 4 mwaka 2018 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Mbali na Malinzi washtakiwa wengine  katika kesi ni  Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, Mhasibu wa TFF,  Nsiande Mwanga, Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh. 43,100,000.


Hivyo makala MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF

yaani makala yote MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mahakama-kisutu-yapokea-nyaraka-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF"

Post a Comment