LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA

LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA
kiungo : LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA

soma pia


LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA

  NA MWAMVUA MWINYI, MKURANGA
KAMANDA wa kanda ya kipolisi Rufiji,mkoani Pwani, Onesmo Lyanga ,amesema wanawatafuta wafugaji aina ya Kibarabaig, ambao walitoroka na mifugo yao, mara baada ya kuwajeruhiwa watu sita ,kijiji cha Kondo Mwilanzi, kata ya Bupu wilayani ,Mkuranga, mkoani Pwani. 

Aidha alieleza, thamani na ukubwa wa mashamba yaliyoharibiwa na ng'ombe aliyejeruhiwa, wanasubiri taarifa kutoka kwa wataalamu wa kilimo na mifugo.

Lyanga aliwaasa wafugaji ,kuacha tabia ya kutumia sheria mkononi kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwemo za jadi ,ili kuepusha madhara makubwa baadae.

"Niyatake makundi ya wakulima na wafugaji kuheshimiana ,kila upande uthamini shughuli ya mwenzake ,na kuacha kushambuliana bila sababu zisizo na tija " alisisitiza Lyanga.
Lyanga alizitaka ,jamii hizo kuishi kwa amani pasipo kutishia amani.

Aliwataja ,walioshambiliwa ni pamoja na Abdallah Kiwembe (34),Shaban Mohammed (49),Nasra Ramadhani,(19),Mustapha Seif (38),Leonard Adolf na Imran Yasne (23)mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo cha SUA kozi ya maabara na Nasra Ramadhani.

Lyanga alitaja chanzo cha ugomvi kuwa ni ng'ombe wa wafugaji kuingia kwenye mashamba ya wakulima watatu ,ndipo walipomkata ng'ombe mmoja mguu na ugomvi ukaanzia hapo.

Baada ya hapo wafugaji walianza kuwashambulia wakulima kisha walitoroka na mifugo yao.

Kufuatia tukio hilo , mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga aliwataka wananchi kuwa watulivu kwani tayari vyombo vya ulinzi vimedhibiti hali ya vurugu na hali ipo shwari.

"Wafugaji hao ambao waliondolewa wilayani Kisarawe walifika kijijini hapo na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kusababisha kutokea kwa vurugu" alisema Sanga.

Nae diwani wa kata ya Bupu Abass Msangule alisema , majeruhi hao walipelekwa hospitali ya wilaya ambapo hali zao zinaendelea vizuri na kuviomba vyombo vinavyohusika na ulinzi kuimarisha ulinzi ili kuwadhibiti wafugaji hao.

Msangule alisema kuwa wafugaji hao walikwenda Kijijini hapo wakiwa na nia mbaya hali ambayo imewafanya wananchi wakose amani tangu kuingia kwa wafugaji hao ambao wana makundi ya ngombe.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa wilaya ya Mkuranga Ndaki Barnabas Mkuranga alielezea, alipokea majeruhi hao,majira ya saa nne usiku wakiwa wamejeruhiwa wawili waliumia kichwani na mwingine kifuani na mguu wa kushoto.
Alisema, hali zilikuwa si nzuri kwani walikuwa wakitoka damu na waliwashona wakawa wanaendelea vizuri ambapo wawili wameruhusiwa mmoja atafanyiwa vipimo zaidi ambaye aliyeumia kifuani ili afanyiwe Xray na ultra sound.

Nae mmoja wa majeruhi wa tukio hilo Abdallah Rashid ambaye ni mkazi wa Mbagala alieleza, yeye alikwenda Mkuranga kuwasalimia wakwe zake na kadhia hiyo ilimkuta wakati alipokwenda dukani kununua vocha .

"Ghafla wakatokea wafugaji hao huku wakimuuliza kama ameonga ng'ombe aliyekatwa mguu akajibu hajaona ghafla wakamvamia na kuanza kumpiga kwa kutumia gongo kichwani.


Hivyo makala LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA

yaani makala yote LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/lyanga-tunawasaka-wafugaji-aina-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA"

Post a Comment