LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU

LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU
kiungo : LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU

soma pia


LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imejumuika na taasisi zingine kuadhimisha wiki ya jeshi la zimamoto na uokoaji kitaifa inayofanyika Jijini Dodoma tarehe 29 Agosti hadi 01 Septemba 2018. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda, funga king’amua moto kwenye kiwanda chako.” 

Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (MB) ambaye alitembelea banda la TMA na kuwapongeza kwa usahihi wa hali ya juu wa utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni na kuwataka waendelee kuboresha ili kufikia viwango vya  juu zaidi ya  walipo kwa sasa. 

Mhe. Lugola aliweza kupata maelezo mafupi kutoka kwa meneja wa TMA kanda ya kati  Bw. Waziri Omari Waziri ambapo alieleza kuwa taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa shughuli za uokoaji na zimamoto, akitolea mfano taarifa za upepo mkali ambao kwa kiasi kikubwa unaweza kusababisha moto kusambaa kwa  kasi (eneo kubwa) au hata kwa watumiaji wa bahari au ziwa kuathirika na mawimbi makubwa vile vile taarifa ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika eneo husika zinasaidia vikosi vya uokoaji kujipanga na vifaa na njia ya uokoaji kutokana na hali ya hewa ya eneo husika. 

Aliongezea kuwa mchango wa taaarifa za hali ya hewa katika kukuza uchumi wa maendeleo ya viwanda ni pamoja na kutambua hali ya hewa ya eneo husika ili kujua namna ya kuwekeza, mfano mwelekeo wa upepo hii inasaidia kujua jinsi ya kuelekezea uchafu (moshi), kiasi cha uzalishaji kama vile vinywaji baridi kwa kipindi cha baridi au joto, usafirishaji wa mazao ya viwandani hutegemea hali ya hewa ya wakati huo sambamba na miundo mbinu mfano kipindi cha mvua kubwa ambacho husababisha uharibifu wa miundo mbinu hivyo ni vyema mwekezaji akatafuta njia mbadala ya usafirishaji na mengine mengi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akipata maelezo kutoka kwa meneja wa TMA kanda ya kati Bw. Waziri Waziri katika banda la TMA kwenye maadhimisho ya wiki ya zimamoto na ukoaji, mkoani Dodoma.
Meneja wa TMA kanda ya kati Bw. Waziri Waziri akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la TMA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mtaalamu kiutoka TMA kanda ya kati Bw. Zeno Chaula akifafanua jambo kwa mwananchi aliyetembelea banda la TMA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Wanafunzi wakipata Elimu ya umuhimu wa tarifa za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali walipotembelea banda la TMA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Hivyo makala LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU

yaani makala yote LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/lugola-usahihi-wa-utabiri-wa-hali-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "LUGOLA: USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI WA KIWANGO CHA JUU"

Post a Comment