JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI

JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI
kiungo : JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI

soma pia


JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI
WAKAZI wa kijiji cha Madege, kata ya Dutumi Kibaha Vijijini ,wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa zahanati hali inayosababisha kufuata huduma ya afya katika zahanati ya Dutumi ,umbali wa km .5-7.

Aidha wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa kutoka kijiji cha Madege hadi kituo cha afya Mlandizi hutumia km.45 jambo ambalo ni kero kwao.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo ,mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amechangia mifuko ya saruji 80 pamoja na diwani wa kata ya Dutumi Mkali Kanusu amechangia mifuko ya saruji 20 ambayo itasaidia kuanza kwa ujenzi wa zahanati kijijini hapo .

Wakipokea msaada huo ,baadhi ya wakazi hao  akiwemo Nassoro Malolela na Nuru Shaban walisema wanataabika kukodi usafiri wa pikipiki kwa sh.10,000 na baiskeli kwenda zahanati ya Dutumi .

Malolela alisema, kusafiri km.5 kufuata huduma hiyo Dutumi ni umbali mrefu kwakuwa wajawazito wanaokwenda kujifungua na watoto hupata shida hasa wakati wa mvua na nyakati za usiku .

"Fikiria mjamzito ama umeshikwa na uchungu unakaaje kwenye pikipiki au baiskeli ,tunapata shida sana " alisisitiza Nuru .

Nae mganga mfawidhi wa zahanati ya Dutumi Pius Gwade, alisema wagonjwa wanaopata rufaa kutoka kijiji cha Madege hupata shida kuwasafirisha kwakuwa hutoka kijiji km.5-7 kufika Dutumi na kuwatoa Dutumi km.45 kwenda Mlandizi.

Awali diwani Kanusu alisema ,Jumaa aliahidi kupeleka mifuko hiyo ya saruji baada ya kufanya ziara ya kawaida kijiji cha Madege na kufikishiwa kero hiyo.

Akikabidhiwa mifuko hiyo ya saruji ,mwenyekiti wa kijiji cha Madege Iddi Msiga alielezea ,kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo itakuwa mkombozi katika kupata huduma za afya.

Alisema ,mkutano wa kijiji umekubaliana kila mkazi kushiriki kuchangia ambapo wameshafikisha sh.400,000 na wanaendelea na michango ili kukamilisha adhma yao.

Wakati huo huo ,Jumaa pia ,alimsaidia Halima Nassoro( 65 ),mabati 20 kwa ajili ya kuezeka nyumba yake ambayo imeezekwa kwa nyasi na kupitisha maji wakati wa mvua .

Halima ,alimshukuru mbunge huyo kwa jitihada zake na kujitolea misaada kwa makundi maalum ikiwemo wazee.
 Bibi Halima Nasorro (65) mkazi wa Dutumi akikabidhiwa mabati 20 kutoka kwa mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa wilayani Kibaha leo.
Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa wilayani Kibaha leo kikabidhi mifuko ya saruji kwa niaba ya mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,diwani wa kata ya Dutumi Mkali Kanusu (kushoto )kwa  Mwenyekiti wa kijiji cha Madege Iddi Msiga (wa pili kulia) na wa kwanza kutoka kulia ni katibu wa mbunge wa Kibaha Vijijini.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Dutumi ,dokta Pius Gwade akizungumza na waandishi wa habari.


Hivyo makala JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI

yaani makala yote JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/jumaa-awaunga-mkono-wakazi-wa-madege.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI"

Post a Comment