JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO

JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO
kiungo : JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO

soma pia


JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo alipokuwa akiapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,katika viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa.

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amewaapisha wakuu wa wilaya wapya wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na Zainab Kawawa wilaya ya Bagamoyo na kutoa maagizo 16 kwa wakuu wa wilaya zote ili kutekeleza majukumu yao. Agizo kubwa ni kuhakikisha kila mkuu wa wilaya anasimamia mapato na kufikia asilimia zaidi ya 25 ifikapo septemba mwaka huu.

Pamoja na hilo ,Ndikilo  amewataka wamiliki wa makampuni kuhakikisha wanakata namba za utambulisho wa biashara TIN ndani ya mkoa badala ya kukatiwa Dar es Salaam kama baadhi yao yanavyofanya na kusababisha kuunyima mkoa mapato. Hafla ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya ilifanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa vilivyopo wilayani Kibaha .

Ndikilo alisema wakuu wa wilaya wanapaswa kufanyia kazi suala la makusanyo na kutoa rai kushirikiana na halmashauri kufikia si chini ya asilimia 25. Alitoa rai kwa wakuu hao wa wilaya, kudhibiti na kusimamia vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo mchanga na kokoto ili kujua vinaingiza mapato kwa kiasi gani .
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Zainabu Kawawa alipokuwa akiapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,katika viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa. (picha na Mwamvua Mwinyi).

"Kuhusu taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG halmashauri zote za mkoa zimepata hati safi lakini msibweteke simamieni sekta zote ili tuendelee kupata hati hizo.

Alimtaka Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,kudhibiti magendo kwenye bandari bubu ambapo kwa Bagamoyo ziko 19 ambazo zinainyima serikali mapato na bidhaa hizo zinaweka rehani maisha ya wananchi kwani hazikaguliwi. Aidha alitaka Jokate na Zainab kwenda kuuliza kwenye maeneo yao kama kuna kamati za amani na endapo hakuna waunde kamati hizo.

“Hakikisheni mnadhibiti migogoro ya ardhi, wakulima na wafugaji kwani kwa mkoa wa Pwani damu iliwahi kumwagika kwenye wilaya za Bagamoyo, Kisarawe, Rufiji na Chalinze "

Ndikilo aliomba nguvu iongezwe ili kuepuka adha hiyo kwa wakati mwingine.


Alisisitiza utunzaji wa hifadhi ya misitu na kuilinda ili isivamiwe na kukabili uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukata mkaa,kuni na mbao .


Katika hilo ,alimuasa Jokate na Zainabu kwenda kusimamia hifadhi ya misitu mikubwa ya Kazimzumbwi -Kisarawe na Uzigua na Ruvu Kusini na Kaskazini-Bagamoyo.

“Nasisitiza maelewano baina ya viongozi wa ngazi mbalimbali kwani baadhi yao hawaelewani hili ni tatizo ambalo halipaswi kuendelea kwani wanaoumia ni wananchi ambao wanapaswa kuongozwa,” alisema Ndikilo.

Kuhusu sekta ya maji ,alimuagiza mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate kumsimamia mkandarasi wa maji kutoka Mloganzila kwenda Kisarawe ili akamilishe kazi kwa wakati .

Ndikilo alisema tatizo la maji ni kubwa wilayani humo hivyo ahakikishe anakuwa mstari wa mbele kushirikiana na mkoa kuusukuma mradi huo ukamilike ili kumtua ndoo mama kichwani.

Kwa upande wao, Jokate Mwegelo na Zainab Kawawa walisema wamepokea maagizo yote na watayafanyia kazi. Jokate alieleza ,hatomuangusha mh.Rais,na wananchi wa Kisarawe na kudai hajaenda kutengua tolati bali amekwenda kuitimirisha,na kuwaomba wote wakutane kazini.


Hivyo makala JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO

yaani makala yote JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/jokate-na-kawawa-waapishwa-pwani-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JOKATE NA KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO"

Post a Comment