title : DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
kiungo : DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania akizungumza na viongozi na wanachama wa mikoa miwili ya CCM Pemba katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Mkoa wa Kusini Pemba.
Na.Is-haka Omar.- Zanzibar..
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania
Dk.Bashiru Ally amesema Chama hicho kinadhibiti mianya
ya ubadhilifu wa rasilimali fedha na mali zake ili kijitegemee
kiuchumi.
Alisema endapo rasilimali hizo zitatumika vizuri na
kuanzishwa kwa miradi mingine mikubwa ya uzalishaji wa
kipato katika ngazi mbali mbali za chama na jumuiya kwa
kuwanufaisha wanachama wote badala ya watu wachache.
Kauli hiyo aliitoa jana katika mwendelezo wa ziara yake
kisiwani Pemba wakati akizungumza na viongozi na
wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Mikoa Miwili
katika ukumbi wa Fidel Castro uliopo, Mkoa wa Kusini
Pemba.
Dk.Bashiru alieleza kuwa lengo la kusimamia dhana ya
ukuaji wa uchumi ndani ya chama kupitia vyanzo vyake vya
mali na fedha ni kukiondosha chama katika mazoea ya
kutegemea ufadhili wa watu wenye fedha wanaokuwa na
malengo ya kujinufaisha wenyewe kisiasa.
Pia aliyataja malengo mengine kuwa ni uimarishaji wa
maslahi ya watumishi wa CCM na jumuiya zake kwani bado
maslahi yao ni ya kiwango cha chini ambayo hayaendani na
hadhi ya taasisi yenyewe.
“ Kwa miaka mingi chama chetu kimeondoka katika misingi
ya kujitegemea na badala yake kujitokeza kwa watu wenye
fedha kukichangia chama wakati wa uchaguzi na mazoezi
mengine ya kitaasisi, sasa katika mageuzi haya ya kimuundo
tuna dhamira ya chama chetu kukiondosha uko na tukaweza
kutumia mali zetu wenyewe kujiendesha kitaasisi.”
Alifafanua Dk.Bashiru.
Alieleza kuwa malengo hayo yakifanikiwa utakuwa ni
ushindi mkubwa kwa wanachama wa CCM wote kwani tabia
za rushwa na makundi ya kusaka nafasi za uongozi kwa
kutumia fedha yatakuwa yamedhibitiwa.
Aliwataka viongozi wote wa taasisi hiyo kuunga mkono
malengo hayo kwa kuhakikisha wanapunguza matumizi
holela ya fedha na badala yake waanzishe miradi
itakayowasaidia kujiendesha ili kulinda heshima na hadhi ya
CCM mbele ya jamii.
Pamoja na hayo alizitaka jumuiya zote hasa ya umoja wa
vijana (UVCCM) kuhakikisha wanakuwa wabunifu kwa
kutumia rasilimia walizonazo kwa kuanzisha miradi
mikubwa ya kilimo, uvuvi na viwanda vidogo vidogo ili
vijana wajiajiri wenyewe.
Katibu Mkuu huyo Dk.Bashiru aliweka wazi msimamo wa
Chama Cha Mapinduzi kuwa wale wote waliohusika na
kutapeli na kujimilikisha mali za taasisi hiyo kinyume na
utaratibu wote watachukuliwa hatua za kisheria.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla
Juma Mabodi alisema wanachama wote wana haki ya
kuunga mkono mambo mema yanayotekelezwa na taasisi
hiyo kwa nia ya kuongeza ufanisi.
Alisema wakati wa vyama vya ukombozi vya ASP na TANU
viongozi wa wakati huo walifanikiwa kupanga mambo ya
maendeleo yaliyodumu kwa muda mrefu kutokana na umoja
na mshikamano waliokuwa nao hasa katika masuala ya
kuvijenga kimaendeleo vyama vyao.
Dk. Mabodi alieleza kuwa suala la uzalendo katika
kusimamia maslahi ya kitaifa ni jambo muhimu hasa kwa
viongozi wanaoaminiwa na kupewa dhamana za kuongoza
jamii.
Akizungumzia ushindi wa CCM visiwani Zanzibar mwaka
2020 alisema mpaka sasa Zanzibar hakuna upinzani bali
kuna vikundi vidogo vidogo vya watu wanaojivisha joho la
upinzani wakati wao ni madalali wa kisiasa waliofilisika
kifikra.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema CCM itashinda kisayansi
kutokana na serikali zake kutekeleza mahitaji ya wananchi
wa mijini na vijijini kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya mwaka 2015/2020.
Hivyo makala DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
yaani makala yote DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dkbashiru-asema-wanaohujumu-mali-za-ccm.html
0 Response to "DK.BASHIRU ASEMA WANAOHUJUMU MALI ZA CCM WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA."
Post a Comment