DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU.

DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU.
kiungo : DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU.

soma pia


DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU.

 Picha mbalimbali za simu.
 Wanafunzi wa kozi fupi wanaosoma taaluma ya mafundimchundo wa simu za mkononi wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mawasiliano kutokana jeshi la polisi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Taasisi ya Teknolojia (DIT)
 Mratibu wa mafunzo wa kozi fupi kwa mafundimchundo simu za mkononi Dkt. Petro Tesha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa kozi mpya kwa mafundi simu.
Mwanafunzi wa kozi fupi kwa mafundi simu akizingumza na waandishi wa habari.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wamenzisha mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya mafundi simu za  mkononi baada ya kubaini idadi kubwa ya mafundi kutokuwa na elimu na kuisababisha sekta ya mawasiliano kukabiliwa na changamoto.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kozi ya mafundisanifu simu za mkononi jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya  DIT Profesa Preksedis Ndomba, amesema kuwa wamejipanga kutoa mafunzo hayo kwa uweledi.

Prof Ndomba amesema kuwa utoaji wa mafunzo ya kozi fupi kwa mafundi simu itasaidia sana watu kupeleka simu zao kwa mafundi wenye uwezo na uweledi katika utengenezaji wa simu.

"Tumefanya uzinduzi rasmi wa kozi fupi kwa mafundimchundo wa simu za mkononi jambo ambalo litasaidia mafundi simu kufanya kazi yao kitaalamu na kupata mafanikio" amesema Prof Ndomba.

Amesema kuwa utoaji wa mafunzo kwa  mafundi simu itasaidia sana katika kuboresha utendaji jambo ambalo litaleta chachu ya maendeleo.

Prof Ndomba amefafanua kuwa tayari wamefanikiwa kupata vifaa vya kisasa ambavyo vinatumika kutolea mafunzo ya kozi kwa mafundimchundo wa simu za mkononi.

Mratibu wa Mafunzo ya mafundimchundo wa simu za Mkononi Dkt. Petro Tesha, amesema kuwa kabla ya kufanikisha utoaji wa mafunzo hayo, novemba I5, 20I6 walikutana na wadau mbalimbali wa mawasiliano kwa ajili ya kutatua changamoto za utengenezaji wa simu.

Dkt. Tesha amesema kuwa baada ya kutambua changamoto za mafundi simu, wameamua kuanzisha kozi fupi ambayo itakuwa msaada katika kufanikisha utendaji wa kazi zao.

"Lengo letu ni kuthbitisha mafundi simu waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kutengeneza simu kupitia vifaa bora" amesema Dkt. Tesha.

Dkt. Tesha amefafanua kuwa mafunzo hayo yatatolewa kuanzia mwezi mmoja, miwili pamoja na wiki mbili.

Amesema mwanafunzi baada ya kumaliza kozi yake na kufanya vizuri atapatiwa cheti cha kumaliza masomo.

"Ni vizuri mafundi simu waje kusoma kozi hii muhimu kwao, kwani wataweza kutambuliwa na kupatiwa leseni jambo ambalo litamwezesha kufanya kazi popote Tanzania" amesema Dkt. Tesha.

Msimamizi wa Uharifu wa Mtandao kutoka Jeshi la Polisi, Kamishena wa Polisi Forensics, Eng. Shabani Hiki, amesema kuwa hivi karibu waharifu wamekuwa wakitumia mbinu mpya za uharibifu kwa kutumia mitandao ya simu.

Eng. Hiki amesema kuwa kutokana na uharifu huo jeshi la polisi limekuwa likifanya juhudi ili kuhakikisha uharifu huo unaondoka.

"Mafunzo haya yatasaidia sana katika kudhibiti uharifu wa mtandaoni kupitia simu, kwani baada ya mafunzo mafundi simu watakuwa na uwelewa mkubwa pamoja na sheria" amesema Eng. Hiki.

Hata hivyo ameeleza kuwa kuna baadhi ya mafundi simu wamekuwa wakifanya udanganyifu mkubwa katika ufundi wao kwani wamekuwa wakibadilisha vifaa vya baada ya simu kuibiwa.

Amesema kuwa baadhi ya mafundi simu wamekuwa wakifanya kazi na waharifu bila kujua kufanya hivyo ni kinyume na sheria za mawasiliano.

Eng. Hiki amebainisha kuwa asilimia kubwa ulimwengu wa sasa unatumia teknolojia, kwani kwa mujibu takwimu za hivi karibuni unaonyesha watumiaji wa simu hapa nchini wapo bilioni 59 ambapo sawa na asilimia 65.

Hata hivyo TCRA wameeleza kuwa kozi hiyo itakuwa chachu maendeleo kwa mafundi simu katika kutatua changamoto zinazojitokeza.

Kozi hiyo itawapa elimu mafundi simu na kulinda mtumiaji wa simu za mkononi jambo litakuwa rafiki.

Baada ya kutolewa mafunzo hayo kutakuwa na utaratibu wa kutolewa leseni kwa mafundi simu ambao waliokizi vigezo.

Katika kufanikisha utolewaji wa mafunzo hayo wanafunzi 72 wamedhaminiwa na TCRA ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.

Mafunzo ya muda mfupi kwa wanafunzi wa kozi fupi kwa mafundimchundo wa simu za mkononi yanatolewa katika Chuo cha DIT.

DIT ni taasisi iliyoanzishwa kwa sheria ya bunge namba 6 ya mwaka I997 lengo ni kutoa elimu taaluma ya uhandisi, kufanya Utafiti pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.











Hivyo makala DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU.

yaani makala yote DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dit-waanzisha-mafunzo-ya-muda-mfupi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DIT WAANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA MAFUNDI SIMU."

Post a Comment