title : DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda
kiungo : DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda
DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema atoa agizo la kukamatwa kuwekwa ndani Diwani wa Kata ya Kitunda Nice Gisunte (CHADEMA) kufuatia diwani huyo kumzuia Mkuu wa wilaya ya Ilala kutekeleza majukumu yake katika ziara ya kutatua kero za wananchi Jimbo La UKONGA.
Akitoa agizo hilo Sophia Mjema aliamuru awekwe ndani masaa 48 diwani huyo kuanzisasa baada diwani huyo kuingilia ziara ya mkuu wa wilaya ya kutatoa kero za wananchi.
"Mimi ndio MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya uwezi kunizuia kuongea katika Wilaya yangu natekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi pia namwakilisha Rais John Magufuli kuakikisha Maendeleo yanakuwa wewe ni Diwani CHADEMA pia unatelekeza ilani ya CCM uwezi kunizuiya kuzungumza na wananchi polisi kamata weka ndani "alisema Mjema.
Kufuatia agizo hilo Askari kanzu walimkata diwani Nice na kuondoka naye majira ya saa Saba .
Wakati huohuo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amegoma kupokea Mradi wa maji wa Kitunda Kipera kufuatia mradi huo kujengwa chini ya Kiwango.
Mjema amewaagiza Mkandarasi wa Sk Building Civil Engineering Work Ltd kujenga upya Mradi huo kufuatia kujengwa chini ya kiwango.
Alisema Mradi huo wa maji umegharimu shilingi milioni 50 fedha iliyotumika shilingi milioni 38 kisima kimechimbwa mita 80 badala mita 100.
"Mradi wa wananchi hivyo lazima uwe mzuri
wananchi waone juhudi za Serikali yao ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli na kutekekeza kauli mbiu ya hapa kazi "alisema.
Aidha pia aliwataka wakazi wa Jimbo la UKONGA kutoa ushirikiano katika kurasimisha makazi yao kwa ajili ya kupimiwa kwa gharama ya shilingi 250,000 bei ya Serikali iliyotangazwa na WAZIRI wa Ardhi William Lukuvi.
Pia aliwatoa hofu wananchi wa Jimbo la Ukonga Serikali yao sikivu amna nyumba zitakazo vunjwa katika wilaya ya Ilala ila wasikae mabondeni ..
Hivyo makala DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda
yaani makala yote DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dc-mjema-atoa-agizo-la-kuwekwa-ndani.html
0 Response to "DC Mjema atoa agizo la kuwekwa ndani Diwani wa Kitunda"
Post a Comment