title : BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11
kiungo : BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11
BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11
John Walter, Babati
Mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba Mjini Babati mkoani Manyara, maarfu kama Babati Nyota Search, yanazidi kushika kasi na kuwaibua vijana wengi wenye uwezo mkubwa katika muziki wa kizazi kipya.
Kutoka washiriki 40 mpaka sasa wamebaki washiriki 11 huku mshiriki wa jinsia ya kike akiwa ni mmoja pekee Apple D. Kila wiki anatoka mshiriki mmoja hadi wafike watatu ambao watachuana ili kupatikana mmoja atakaenyakua kitita cha shilingi laki tano pamoja kurekodiwa wimbo mmoja na video.
Akizungumza Chief Jaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Smile Fm Radio ya Babati Juma Msuya amesema mashindano hayo ni fursa tosha kwa washiriki kutambua uwezo walionao katika tasnia ya muziki.
Amesema mpaka sasa amegundua viapaji zaidi ya 20 vya muziki hivyo ni wakati wa wakazi wa Babati kujitokeza na kuwasaidia vijana hao ili kuinua vipaji walivyonavyo.
Msanii Wiliam Stebin Loya [Mono Music] alieimba wimbo wa Jux Looking For you aliomshiriksha Joe Makini ulikuwa kivutio kikubwa kwa mamia ya mashabiki waliokuwa wakishangilia alipokuwa akiimba kwa ufundi wa hali ya juu.
Mashindano hayo yanafanyika kila Jumapili saa tatu usiku na kurushwa live kupitia Babati Cable Tv na Smile Fm Radio.
Hivyo makala BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11
yaani makala yote BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/babati-nyota-search-yashika-kasi-kati.html
0 Response to "BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11"
Post a Comment