title : ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI.
kiungo : ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI.
ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI.
Jeshi nchini uganda limeomba msamaha kutokana na kitendo cha askari wake kuonekana kwenye video akimpiga mwandishi wa habari ambaye alikuwa akitimiza wajibu wake kwenye maandamano ya kushutumu kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine Agosti 20 mwaka huu.
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi (CDF), Jenerali David Muhoozi, ameagiza askari waliohusika kuwapiga wanahabari waliokuwa wakitimiza majukumu yao kukamatwa.
Mbali na hatua hiyo ya jeshi hilo jumuiya ya kimataifa zimeshaanza kuwashutumu askari wa Jeshi la Ulinzi (UPDF) kwa ukatili na manyanyaso ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakiandika habari za kampeni katika Jimbo la Manispaa ya Arua hivi karibuni.
Imeelezwa kuwa kisa cha kukamatwa kwa wanasiasa na kuibuka vurugu katika maeneo mengi ya jiji la Kampala Jumatatu.
Msemaji wa UPDF Brigeduia Richard Karemire katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari amesema uongozi wa jeshi unalaani ukatili uliofanywa na askari wake.
“Uongozi wa UPDF umefahamishwa kuhusu utendaji kazi usiozingatia weledi wa askari wake waliowasumbua wanahabari waliosambazwa kwa ajili ya kufuatilia operesheni ya pamoja katika jiji Jumatatu ya Agosti 20, 018,” ilisema sehemu ya taarifa Brigedia Karemire iliyosambazwa Jumanne.
“UPDF linapenda kueleza kwamba halijafurahishwa na tabia hiyo iliyofanywa na askari hao binafsi, na kwa sababu hiyo Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi (CDF) ameamuru wakamatwe na waadhibiwe.
Waandishi waliokumbana na mkono katili wa askari wa vikosi vya usalama ni wanahabari wanne wa televisheni ya NTV; Juma Kiirya, Herbert Zziwa, Ronald Muwanga, Ronald Galiwango, na wenzao Julius Bakabaage (NBS), James Akena (Reuters), Samuel Kyambadde (Metro FM) na Richard (Ghetto TV).
Hivyo makala ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI.
yaani makala yote ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/askari-aliyempiga-mwandishi-matatani.html
0 Response to "ASKARI ALIYEMPIGA MWANDISHI MATATANI."
Post a Comment